Habari Tanzania - http://www.habaritanzania.com
Mwanafunzi Aliyefanikiwa Kurusha Matangazo Ya FM Ajitokeza Hadharani
http://www.habaritanzania.com/articles/431/1/Mwanafunzi-Aliyefanikiwa-Kurusha-Matangazo-Ya-FM-Ajitokeza-Hadharani
By Prosper Kwigize
Published on 07/3/2006
 

Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Maragalasi wilayani Kibondo ambaye mtandao huu ulitangaza kufanikisha kwake kuunganisha mitambo ya redio na kurusha matangazo amejitokeza hadharani kuomba misaada.


Kibondo
Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Maragalasi wilayani Kibondo ambaye mtandao huu ulitangaza kufanikisha kwake kuunganisha mitambo ya redio na kurusha matangazo amejitokeza hadharani kuomba misaada.
 
 Akiongea na mwandishi wa HabariTanzaniacom kijana huyo Eliud Kajuni amesema amekuwa akipata hofu kubwa kwa kudhani kuwa angeweza kuchukuliwa hatua kwa kitendo chake cha kurusha matangazo yake kama sehemu ya majaribio.
Mwanafunzi Eliud Kajuni, aliyefanikiwa kuonesha kipaji cha kuunda mitambo na kurusha matangazo ya redio katika mjini wa Kibondo mkoani Kigoma hivi karibuni katika FM 108Mhz (Anaomba msaada wa zana za majaribio ili kupanua uvumbuzi wake) (Picha na Prosper Kwigize)

 Amebainisha kuwa tangu alipotangazwa na mtandao wa HabariTanzania.com amekuwa akipatiwa pongezi za hali ya juu ambazo zimemtia hamasa na kuamua kukiweka kipaji chake hadharani bila woga.
 
 Amefafanua kuwa baadhi ya walimu, wanafunzi na hata wazazi wange walikuwa wakimzuia kufanya hivyo ingawa iliendelea kwa uficho hadi mtandao wa HabariTanzania.com ulipomuibua na kutangaza habari zake.
 
 Bw. Kajuni amesema anadhamilia kukuza kipaji chake kwa kujipatia elimu ya mitambo na utafiti lakini hadhani kama ataweza kutokana na kutokuwa na uwezo, na hivyo anaomba serikali imsadie kupata masomo ya chuo cha ufundi chenye hadhi.
 
 Ameongeza kuwa pamoja na kuendelea na elimu yake ya sekondari anadhani kuwa ipo haja ya kuijiunga na vyuo vya vipaji maalumu, kama vile VETA na vinginevyo.
 
 Ameongeza masikitiko yake kuwa hadi sasa hana zana za kutosha kufanyia mazoezi hali inayomtatiza anapojaribu kuboresha mtambo wake wa matangazo, amesema zana anazohitaji ni pamoja na redio casstte kubwa band 4, kipaza sauti 1, waya mita 20 pamoja na mashine ndogo ya umeme.