Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mwanafunzi Aliyefanikiwa Kurusha Matangazo Ya FM Ajitokeza Hadharani
Mwanafunzi Aliyefanikiwa Kurusha Matangazo Ya FM Ajitokeza Hadharani
By Prosper Kwigize | Published  07/3/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Kibondo
Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Maragalasi wilayani Kibondo ambaye mtandao huu ulitangaza kufanikisha kwake kuunganisha mitambo ya redio na kurusha matangazo amejitokeza hadharani kuomba misaada.
 
 Akiongea na mwandishi wa HabariTanzaniacom kijana huyo Eliud Kajuni amesema amekuwa akipata hofu kubwa kwa kudhani kuwa angeweza kuchukuliwa hatua kwa kitendo chake cha kurusha matangazo yake kama sehemu ya majaribio.
Mwanafunzi Eliud Kajuni, aliyefanikiwa kuonesha kipaji cha kuunda mitambo na kurusha matangazo ya redio katika mjini wa Kibondo mkoani Kigoma hivi karibuni katika FM 108Mhz (Anaomba msaada wa zana za majaribio ili kupanua uvumbuzi wake) (Picha na Prosper Kwigize)

 Amebainisha kuwa tangu alipotangazwa na mtandao wa HabariTanzania.com amekuwa akipatiwa pongezi za hali ya juu ambazo zimemtia hamasa na kuamua kukiweka kipaji chake hadharani bila woga.
 
 Amefafanua kuwa baadhi ya walimu, wanafunzi na hata wazazi wange walikuwa wakimzuia kufanya hivyo ingawa iliendelea kwa uficho hadi mtandao wa HabariTanzania.com ulipomuibua na kutangaza habari zake.
 
 Bw. Kajuni amesema anadhamilia kukuza kipaji chake kwa kujipatia elimu ya mitambo na utafiti lakini hadhani kama ataweza kutokana na kutokuwa na uwezo, na hivyo anaomba serikali imsadie kupata masomo ya chuo cha ufundi chenye hadhi.
 
 Ameongeza kuwa pamoja na kuendelea na elimu yake ya sekondari anadhani kuwa ipo haja ya kuijiunga na vyuo vya vipaji maalumu, kama vile VETA na vinginevyo.
 
 Ameongeza masikitiko yake kuwa hadi sasa hana zana za kutosha kufanyia mazoezi hali inayomtatiza anapojaribu kuboresha mtambo wake wa matangazo, amesema zana anazohitaji ni pamoja na redio casstte kubwa band 4, kipaza sauti 1, waya mita 20 pamoja na mashine ndogo ya umeme.
 

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by Haji Khamis)
    Rating
    Well done.
     
  • Comment #2 (Posted by Bekky Mohammed)
    Rating
    Excellent keep moving !
     
  • Comment #3 (Posted by Bruno D Shao)
    Rating
    Serikali imsaidie huju kijana kwani ameonyesha kipaji na ujuzi wa hali ya juu ambao hutokea kwa mara chache na kwa watu wachache.
    Kama akisaidiwa anaweza kuja kuwa asset nzuri kwa taifa letu la baadae.
     
  • Comment #4 (Posted by Goodluck Ole-Medeye)
    Rating
    Tunashukuru kwa taarifa juu ya mafanikio ya kijana huyo. Hata hivyo unaombwa umshauri awasiliane na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwani kuendelea kurusha matangazo hayo ni kosa la jinai. Hiyo ni kwa sababu anatumia masafa ambayo hajapangiwa na hivyo huweza kusababisha mwingiliano na kuvuruga mawasiliano (harmful intereferenece) ya watumiaji halali. Hata kama anataka kurusha kwa majaribio ni lazima apate kibali cha Mamlaka kutumia masafa.
    Tunashukuru kwa ushirikiano wako.


     
  • Comment #5 (Posted by Mkubwa)
    Rating
    Kijana ametenda vena na yapaswa asaidiwe na serikali ya tanzania
     
  • Comment #6 (Posted by Msomaji)
    Rating
    Utoaji habari juu ya kijana huyo haukukamilika. Mwandishi angeeleza ni nini hasa alichofanya huyo kijana katika uvumbuzi wake huo wa kurusha matangazo; alitumia zana ghani; na katika msaada anaouhitaji kwa habari ya zana za kuendeleza majaribio ya uvumbuzi wake ni nini hasa anahitaji (taja vitu bayana).

    Poor reporting!
     
  • Comment #7 (Posted by Mbwambo W. M)
    Rating
    Well done Eliud & keep it up!
     
  • Comment #8 (Posted by herry)
    Rating
    i think is the good chance for governmement to give this man sponsership in this technology because he can became a basic pillar in nation.
     
  • Comment #9 (Posted by Mrs. S. Takadiri, Dodoma)
    Rating
    I joined with his job and ask government to give him support.
     
  • Comment #10 (Posted by Charles Mwasha)
    Rating
    Excelent! Mambo alofanya kijana niyakustaajabisha sana na yanahitaji pongezi. Hofu yangu ni kwamba pamoja na mafanikio haya usije shangaa anazuiwa kuendelea na utafiti wake. si unajua Waafrika tunasifu vya wazungu tu !
     
  • Comment #11 (Posted by Iddy Mkwama)
    Rating
    tunashukuru sana kwa kutuhabarisha yanayojiri huko kibondo huyu kijana anapaswa kuendelezwa ili aweze kufanya mambo makubwa zaidi tanzania bado inahitaji wabunifu kama hawa akiendelezwa atakuja kufanya makubwa zaidi ya haya so aendelezwe kazi nzuri kwizige big up!
     
  • Comment #12 (Posted by johansen)
    Rating
    hongera, selikari ya sasa itakusaidia maana si kama ile ilopita.
     
  • Comment #13 (Posted by king)
    Rating
    Safi sana asaidiwe haraka wavumbuzi kama hawa wanatafutwa duniani kote
     
  • Comment #14 (Posted by washawasha)
    Rating
    Naomba kumuuliza huyo dogo,
    1.Hivyo vifaa viko nyumbani kwao ama alifanyia wapi hayo majaribio?
    2.na hivyo baadhi ya vifaa alivyonavyo ni vingapi na vinaitwaje?
    3.na yeye ana short ya nini ili aweze kukamilisha zoezi lake hilo????
    Asante
     
  • Comment #15 (Posted by Fikirini Ambuje)
    Rating
    Eliud, hongera sana kwa juhudi na mafanikio yako pia Prosper kwa kumuibua kijana huyu. Ni kweli kabisa kijana anapaswa kusidiwa iwe serikali au wenye uwezo. Mengi ya jinsi hii tumekuwa tukiyasikia na kuyaona lakini hayaendelezwi. Wapo vijana Arusha pia tulionyeshwa wanataka kurusha ndege sijui imefikia wapi. Kipindi cha marehemu Edward Moringe Sokoine akiwa waziri mkuu alialika wale wote wenye vipaji na uwezo wa kufanya ugunduzi waende Dodoma wakajisajili na serikali ingewawezesha na kuwasidia ili wafanikishe kwa faida ya nchi. Zoezi hilo liliishia tu hewani hatukusikia tena, pengine ilikuwa wakati wa kurudia tena.
     
  • Comment #16 (Posted by Brown Hasunga)
    Rating
    LET this talented and gifted youngs given all neccessary support by both govermnent particulary Tume ya sayansi na Techolojia which has a mandate to support this .
    I encourage the boy to keep on thinking not only asking the support but being more creative to manage such challenges. even the Former scientist used their own initiatives to win their problems.
    problems should be a way to find a solution to a particular problems,
    wish u all the best as we struggle to have our own scientists in TANZANIA
     
  • Comment #17 (Posted by mamapeiraa)
    Rating
    serikali iangalie uwezekano wa kumsaidia huyo kijana
     
  • Comment #18 (Posted by wewe)
    Rating
    hi
     
Submit Comment


Article Options
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  3. Is Tanzania a safe place to invest?
  4. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
  5. Nitaendelea kugombea nafasi za kisiasa- Balozi Karume
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Linda Garner
  4. Nthelezi Nesaa
  5. Marshy Abdu
  6. Prosper Kwigize
  7. Salehe Mmoro
  8. Ramadhan Semtawa
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.