Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Ban Ki-Moon atishwa Dar
Ban Ki-Moon atishwa Dar
By Marshy Abdu | Published  02/25/2009 | Habari za Kitaifa | Rating:
Ban Ki-Moon atishwa Dar

na Mwandishi Wetu

 

WAKATI Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-Moon akitarajia kutua nchini kesho kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, serikali imefichua mpango wa baadhi ya Watanzania kuihujumu ziara hiyo.

Taarifa ya serikali iliyotolewa jana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini ofisi kwake Dar es Salaam, ilieleza kuwa serikali imebaini mpango wa kuhujumu ziara hiyo unaofanywa na baadhi ya makundi ya watu wa ndani na nje ya nchi.

Kwa mujibu wa Membe, wizara yake imepata tetesi hizo ambazo zimezagaa jijini Dar es Salaam, zinazoeleza kuwa kundi moja wapo linalotarajiwa kushiriki katika mpango huo ni la wazee kutoka Kisiwa cha Pemba, wanaotaka kisiwa hicho kijitenge.

Wazee hao walishawahi kupeleka barua za kusudio lao la kutaka kisiwa hicho kijitenge katika ofisi za Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Hata hivyo, ombi lao hilo liligonga mwamba baada ya maofisa wa UNDP kuwaelekeza wazee hao kwenda Tume ya Haki za Binadamu, lakini badala yake waliposikia ujio wa Ki-Moon hapa nchini waliamua kujipanga upya na kubuni njia nyingine ya kufikisha ujumbe wao kwa katibu mkuu huyo.

Membe alieleza kuwa, taarifa zinaonyesha kuwa wazee hao wamepanga kuwa na mabango ya kumkashifu Ki-Moon kwa madai kuwa ni mnyanyasaji wa haki za binadamu kutokana na ombi lao kukataliwa na shirika lililo chini ya uongozi wake.

Kwamba wazee hao wamepanga kulala barabarani katika maeneo ya Buguruni, njia ambayo anatarajiwa kupita Ki-Moon na endapo watafanikiwa kuusimamisha msafara wa kiongozi huyo, watamsomea risala yao juu ya azima yao ya kutaka Kisiwa cha Pemba kijitenge.

Wakati kundi la pili la watu walio katika mpango huo, ambalo Membe alilitaja kuwa linaundwa na Watanzania wanaoishi nje ya nchi, limepanga kutumia vyombo vya habari kuandika habari mbaya dhidi ya katibu mkuu huyo.

Membe alisema serikali haijazipuuzia tetesi hizo na imejipanga vilivyo kuhakikisha wale wote waliopanga kuihujumu ziara ya katibu mkuu huyo hawafanikiwi.

“Tunawaomba Watanzania waonyeshe ukarimu, matatizo yetu tuyamalize wenyewe na tusiitumie ziara hii kwa mambo yasiyofaa.

“Wizara imepata taarifa kwamba kuna watu ambao wamepanga kuvuruga ziara hii kwa maana ya kutaka kuingilia programu ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, pasipo kualikwa na pengine kufanya maandamano kinyume cha taratibu na sheria, serikali inalifanyia kazi tatizo hilo,” alisema Membe.

Alisema kama ziara hiyo itahujumiwa na watu hao, basi itakuwa ni aibu kwa taifa pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha - Rose Migiro, ambaye ni mwanamke wa kwanza kutoka Afrika (Tanzania) kushika wadhifa huo.

Aidha, Membe alisema ziara hiyo ya kiongozi huyo ina lengo la kuimarisha mahusiano baina ya Tanzania na Umoja wa Mataifa, hivyo ni vema Watanzania wakaitumia vizuri fursa hiyo badala ya kumpokea kwa mabango na maneno ya kumkashifu.

Alisema Ki-Moon alikuwa na mahusiano mazuri na nchi za Afrika na amehakikisha masuala yote yalilolihusu bara hili yanapewa kipaumbele ili liweze kuwa na maendeleo.

Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa anatarajiwa kuanza ziara yake nchini kesho hadi Jumamosi, kufuatia mwaliko alioupata kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete, walipokutana nchini Marekani mwaka jana.

Akiwa hapa nchini, Ki-Moon atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete na atapata nafasi ya kutembelea miradi inayosimamiwa na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa pamoja na mradi wa majaribio wa One UN.

Aidha, kiongozi huyo kesho kutwa atapata nafasi ya kuelekea visiwani Zanzibar na akiwa huko atazungumza na Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na kuzindua jengo la Umoja wa Mataifa Zanzibar.

Ki-moon baada ya kutoka visiwani Zanzibar atapata nafasi ya kutembelea Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), iliyopo mjini Arusha.

Hii ni mara ya kwanza kwa Ki-Moon kufanya ziara hapa nchini tangu achaguliwe kushika wadhifa huo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.