Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kimataifa  »   Mbeki amjulia hali Balozi Mwambulukutu
Mbeki amjulia hali Balozi Mwambulukutu
By Habari Tanzania | Published  01/5/2008 | Habari za Kimataifa | Unrated
na Mwandishi Wetu


RAIS Thabo Mbeki wa Afrika Kusini, juzi alimtembelea hospitali na kumjulia hali Balozi wa Tanzania nchini humo, Emmanuel Mwambulukutu.

Balozi Mwambulukutu alilazwa hospitalini mjini Pretoria/Tshwane wiki iliyopita baada ya kuvamiwa na kuumizwa na majambazi.

Kabla ya kumtembelea Balozi, Rais Mbeki alimpigia simu na kuzungumza na Rais Jakaya Kikwete, akimwelezea masikitiko yake juu ya tukio hilo la kuumizwa kwa Balozi Mwambulukutu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari jana, Rais Mbeki pia alimweleza Rais Kikwete kuwa mmoja kati ya watu wanaosadikiwa kumshambulia Balozi Mwambulukutu, ameshakamatwa na polisi.

Rais Mbeki alimweleza Rais Kikwete kuwa, majambazi wengine watano bado wanatafutwa kuhusiana na tukio hilo. Aliahidi kuwa polisi wa nchi yake watafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa wote wanapatikana na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Balozi Mwambulukutu aliumizwa wiki iliyopita wakati watu wasiojulikana walipovamia nyumba ambako balozi huyo alikuwa anafanyiwa hafla ya kumwaga, na wakajaribu kuiba gari.

Anatarajiwa kurejea nyumbani karibuni baada ya kuwa amemaliza muda wake wa utumishi wa ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  3. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Nitaendelea kugombea nafasi za kisiasa- Balozi Karume
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Nthelezi Nesaa
  4. Linda Garner
  5. Marshy Abdu
  6. Prosper Kwigize
  7. Salehe Mmoro
  8. Ramadhan Semtawa
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.