Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Jamii  »   Waziri kuwatembelea wafungwa gerezani
Waziri kuwatembelea wafungwa gerezani
By Habari Tanzania | Published  12/22/2007 | Jamii | Unrated
na Hellen Ngoromera


SERIKALI imeanzisha mpango wa maboresho ya sekta ya sheria ili kukabiliana na kero mbalimbali, ikiwemo msongamano wa watuhumiwa magerezani.

Mabadiliko hayo yatahusisha ziara za Waziri wa Sheria na Katiba pamoja na maofisa kadhaa magerezani, ili kuangalia masuala kadhaa yanayohusu wafungwa na mahabusu, hasa kubambikiwa kesi.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Mary Nagu alibainisha hayo juzi wakati alipokuwa akizungumza kupitia Televisheni ya Taifa (TvT) na kusikika kupitia Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD).

Kwa mujibu wa Dk. Nagu, sekta ya sheria ndiyo mhimili wa amani na utulivu nchini, hivyo kupitia mpango huo, masuala mengine kama ubambikizwaji wa kesi na kero nyingine nyingi yatapatiwa ufumbuzi.

Aliongeza kuwa, kutokana na kuanzisha mpango huo, mafanikio yameanza kuonekana kwani hadi sasa kuna majaji 51 tofauti na awali ambako walikuwa nusu ya idadi hiyo.

Pamoja na mambo mengine, alisema serikali imeajiri pia mahakimu wa mahakama za kazi 70, wa mahakama za mwanzo 46, wanasheria 157, imekarabati mahakama za wilaya sita na kuwa kwa sasa ukarabati wa mahakama za hakimu mkazi Shinyanga na Manyara unaendelea.

Kwa mujibu wa Waziri Nagu, ongezeko la mahakimu litasaidia uharakishwaji wa kesi, hivyo kupunguza mlundikano wa watuhumiwa magerezani.

Alisema pamoja na hilo, pia ataanzisha utaratibu wa kutembelea magereza ya Mkoa wa Dar es Salaam, akiambatana na mahakimu, wanasheria, wahusika kutoka Wizara ya Usalama wa Raia na Magereza ili kuangalia mambo mbalimbali, ikiwemo kuwabaini watuhumiwa wanaobambikiwa kesi, ambao wanaweza kuachiwa.

“Suala la ubambikizwaji wa kesi lipo, tutamchukulia hatua za kisheria mtendaji yeyote atakayebainika kujichukulia sheria mkononi,” alisema Waziri Nagu.

Akizungumzia suala la rushwa mahakamani, Dk. Nagu ambaye aliambatana na Naibu Waziri wake, Mathias Chikawe, alisema suala hilo halina mjadala na kuwa serikali italipiga vita ili kuhakikisha wanalitokomeza.

“Ni kweli kuwa kuna mahakimu wachache wanapatikana kwa rushwa, lakini walio wengi wanajitahidi, watakaopatikana na rushwa watanaswa, watendaji wa mahakama waone kuwa wamepewa dhamana kubwa. Dhamana hiyo haiwezi kulinganishwa na sh 100,000,” alisema Waziri Nagu.

Sambamba na hilo, alisema ili kupunguza hali hiyo, wana mpango wa kuanzisha mabaraza ya kata kusaidia masuala mbalimbali ya kisheria. Aliishauri jamii kupunguza uhalifu kwani hali hiyo itasaidia kuepusha msongamano magerezani.

Akijibu swali la msikilizaji John John kutoka Zanzibar, kuhusu uendeshwaji wa kesi unaofanywa kwa lugha ya Kiingereza, Waziri Nagu alisema hilo ni tatizo na kuwa serikali itaangalia utaratibu wa kuliboresha.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  3. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Nitaendelea kugombea nafasi za kisiasa- Balozi Karume
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Nthelezi Nesaa
  4. Linda Garner
  5. Marshy Abdu
  6. Prosper Kwigize
  7. Salehe Mmoro
  8. Ramadhan Semtawa
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.