Habari Tanzania - http://www.habaritanzania.com
Idd el Hajj Sikukuu ya Kiislam baada ya ibada ya hijja
http://www.habaritanzania.com/articles/4262/1/Idd-el-Hajj-Sikukuu-ya-Kiislam-baada-ya-ibada-ya-hijja
By Marshy Abdu
Published on 12/20/2007
 
LEO Wailamu kote nchini wameungana na wenzao duniani kusherehekea Sikukuu ya Idd el Hajj, mbayo husherehekewa baada ya mahujaji kukamilisha ibada ya hijja, kwenye miji mitakatifu ya Makka na Madina

Idd el Hajj Sikukuu ya Kiislam baada ya ibada ya hijja

Na Shabani Matutu

LEO Wailamu kote nchini wameungana na wenzao duniani kusherehekea Sikukuu ya Idd el Hajj, mbayo husherehekewa baada ya mahujaji kukamilisha ibada ya hijja, kwenye miji mitakatifu ya Makka na Madina.

Siku hii ya Idd el Hajj waislamu huitumia katika kufurahi na kumshukuru Mwenyezi Mungu, ikiwa inaambatana na kuchinja wanyama kwa watu wenye uwezo, ikiwa ni Sunna, kama alivyofanya baba yetu Nabii Ibrahimu (AS).

Sikukuu ya Idd huswaliwa swala yake asubuhi sambamba na kumtukuza Allah (SW), na mahali panapofaa kuswaliwa siku hii ni penye eneo kubwa, ingawa pia si vibaya kuswali misikitini.

Kwa mujibu wa mafundisho ya Mtume Muhammad (SAW) ni kwamba inapendeza siku ya Idd watu wa mji wakakusanyika na kusali pamoja kisha wakaungana katika kusherehekea na kufurahia siku hiyo.

Kwenda hijja ni lazima kwa waislam?

Ibada hii ya hijja, ni moja kati ya nguzo tano za Uislam na kwamba wanaopaswa kuitekeleza ni wale wenye uwezo na kwa wale wasiokuwa nao hawalazimishwi kuhiji.

Hii inatokana na ukweli kwamba, Mwenyezi Mungu alishafahamu tofauti ya uwezo miongoni mwetu kabla hata ya sisi wenyewe kuumbwa, hivyo akabainisha kuwa Uislamu ni dini nyepesi si dini ya kushurutishwa kwenye uzito utakaowapa watu tabu kuifuata dini yao.

Hivyo basi, kwenda Makka kwa asiyekuwa na uwezo si dhambi, na ni lazima tu kwa wale waliojaliwa kuwa na uwezo wa mali ya kuwawezesha kukamilisha ibada hiyo.

Ibada ya hijja ilikuwa ikifanywa hata katika nyakati za kipenzi chetu Mtume Muhammad (SAW), na licha ya kuwa Mtume, na kuwa na uwezo wa kwenda kila mwaka, lakini bado hakwenda hijja kila mwaka.

Hijja ni dalili za wazi za uwepo wa Mwenyezi Mungu. Huko kunapatikana kumbukumbu ya kunusurika kuchinjwa kwa Nabii Ismail (AS) na baba yake Nabii Ibrahim (AS), kisa ambacho nitakielezea kwa kifupi kutokana na ufinyu wa nafasi na nina imani wengi mnakifahamu vema.

Historia hii kwa ufupi ni kuwa; katika mwezi wa nane wa Kiislamu, Nabii Ibrahim alioteshwa ndoto ikimtaka amchinje mwanae wa pekee, Ismail (AS). Mwezi huu Nabii Ibrahimu aliutumia kwa kufikiria ndoto ile na ukapewa jina la ‘Mwezi wa Fikra’ (Hanibal).

Mwezi wa 10 wa Kiislamu ndiyo mwezi ambao aliamua kumsimulia mwanae ndoto aliyoiota ya kutaka kumchinja.

Baada ya kusimuliwa ndoto hiyo, Ismail alimwambia baba yake kuwa afanye yale yote aliyooteshwa na Mwenyezi Mungu.

Ismail (AS) alimwambia hivyo baba yake Nabii Ibrahim (AS) kutokana na kuamini kwake kuwa maneno yale yalikuwa ya Mwenyezi Mungu kwa kuwa aliamini nabii wa Mungu hawezi kuota yasiyokuwa ya Mwenyezi Mungu.

Baada ya Ismail (AS) kumkubalia baba yake kufanya kile alichoamrishwa na Mwenyezi Mungu waliondoka moja kwa moja mpaka katika mji unaoitwa Minna.

Walipofika katika eneo hilo, Ismail (AS) alimuomba Mwenyezi Mungu na kisha akamwambia baba yake amfunike usoni ili asimuonee huruma wakati wa kukamilisha amri hiyo ya kumchinja.

Ismail alijifunika usoni na kulazwa kifudifudi, hapo Nabii Ibrahim akaanza kupitisha panga kwenye shingo ya mwanae, lakini halikuweza kukata, na ghafla akasikia sauti kutoka nyuma yake ikisema ‘Allah Akbar, Allah Akbar’.

Nabii Ibrahim alipogeuka, alimuona malaika Jibril akiwa amemshika kondoo aliyekuwa amekuja naye kutoka mbinguni ili amchinje badala ya mwanawe.

Naye Nabii Ibrahimu (AS) aliitikia kwa kusema: “Laa illah, illaa-llah Allah akbar” na kumchukua yule kondoo na kuanza kumchinja badala ya mwanae.

Hapo Mwenyezi Mungu kutokana na Nabii Ibrahim kukubali kumtoa mwanae kama alivyomwotesha, akamuahidi kupata mtoto mwingine wa kiume ambaye alikuwa Is-haka.

Tangu hapo ndipo ikaamuriwa kuwa moja ya mambo yanayotakiwa kufanywa katika hijja na mahujaji ni pamoja na kuchinja mnyama ikiwa ni ishara ya kukumbuka siku hii.

Mambo yanayotakiwa kufanywa siku ya Idd

Ni jambo la heri kwa Muislamu siku ya Idd kuoga, kuvalia nguo nzuri ikiwa ni pamoja na kupaka uturi (manukato) mzuri.

Pia ni siku ambayo inafaa kwa Waislamu kupika vyakula vizuri na vinywaji visivyokuwa na vilevi na walio na uwezo ni sunna kumchinja mnyama aliye bora zaidi kuliko wengine katika mifugo yao.

Hadithi ya Hassan Asibbit (RA) inasema kwamba, Mtume (SAW) ametuamrisha katika Idd mbili kuvaa vizuri zaidi kadiri tuwezavyo, tupake uturi bora zaidi kuliko wote tulionao na tuchinje wanyama wenye thamani zaidi kuliko wote tulionao.

Pia ni sunna kuwatembelea wagonjwa, majirani, yatima, maskini na watu wasiojiweza ikiwa ni pamoja na kupeana zawadi.

Kwa wale Waislamu walio na uwezo wa kuchinja, wawagawie majirani zao wasiokuwa na uwezo chakula ili na wao wapate kusherehekea sikukuu hii.

Muda unaofaa kutolewa Zakatul Fitr umebainishwa kwenye hadithi iliyotolewa na Ibn Umar (RA) ambayo inasema kwamba Mtume (SAW) aliwaeleza watu kuwa watoe Zakatul Fitri kabla ya kuswali ldd el Hajji.

Kulipa Zakatul Fitri mapema kabla ya kuswali Idd au mapema zaidi ya hapo, kutamuwezesha unayempatia kufurahia Idd na Waislamu wengine.

Iwapo itatokea sababu ya msingi kama vile kusahau mpaka Idd ikaswaliwa, basi hana budi kuitoa baada ya swala na iwapo ataacha kutoa kwa makusudi au kwa uzembe basi ajue kutoa kwake huko hakutamnufaisha kwa chochote.

Watu wanaostahili kupewa Zakatul Fitr ni maskini na wasiojiweza kupata chakula pamoja na wale walio chini ya uangalizi na wale walio chini yake ili wajisikie kufurahia Idd na Waislamu wenzao wenye uwezo.

Iwapo Zakatul Fitr atapewa mtu aliye na uwezo na kuachwa asiye nao wote ambao watakuwa wametoa na kupokea Zakatul Fitr hiyo watakuwa wameidhulumu haki ya anayestahili kupewa hivyo watakuwa wamekwenda kinyume na matakwa ya Mwenyezi Mungu.

Sikukuu ya Idd haistahili kusherehekewa kwa kupiga muziki, ngoma, kunywa vilevi na kufanya mambo yaliyokatazwa na Mwenyezi Mungu kwani utakuwa umemuasi.

Siku ya Idd si siku ya kufanya maasi, kwani Mtume (SAW) anasema: “Kumuasi Mwenyezi Mungu siku ya Idd ni sawa na kufanya uasi siku ya kiyama.”