Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Tulumbane vijiweni lakini tuhimize maendeleo – JK
Tulumbane vijiweni lakini tuhimize maendeleo – JK
By Marshy Abdu | Published  12/7/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
Tulumbane vijiweni lakini tuhimize maendeleo – JK
na Maura Mwingira, Mafia


RAIS Jakaya Kikwete amewasihi wanasiasa wenzake kuwahimiza wanachama wao kushiriki katika shughuli za maendeleo kwa faida ya Watanzania wote.

Alisema katika jambo lolote linalohusu maendeleo, wananchi washirikiane pasipo kujali wapo katika chama gani cha siasa, kwa sababu maendeleo hayana siasa.

“Wanasiasa wenzangu tuendelee kusema na kwenye vijiwe vyetu, wewe hufai, mimi nafaa, wewe uko vile huyu yuko vile, lakini tutakapofika kwenye maendeleo yetu haya ni maendeleo kwa manufaa yetu sote,” alisisitiza.

Alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika Wilaya ya Mafia akiwa katika ziara ya kukagua na kuhimiza shughuli za maendeleo mkoani Pwani.

“Tumeunda vyama vya siasa kwa sababu tunataka kuwaletea watu maendeleo, tunataka watu wapate barabara, wapate maji safi na salama, wapate huduma za afya kwa karibu na wapate elimu. Sasa pale tunapoendelea kushughulikia haya naomba sana sote tuungane kuyafanikisha,” alisihi.

Alieleza kuwa mwanasiasa ambaye anayevutia masuala ya maendeleo upande mwingine, hana masilahi ya maendeleo ya watu, bali anatawaliwa na ubinafsi wake.

Alisema tofauti za kisiasa miongoni mwa Watanzania kunawapa fursa ya kuchagua sera bora zaidi , akiona CCM inamfaa zaidi basi atakwenda huko na akiona CUF inamfaa zaidi atakwenda huko.

Alitahadharisha kuwa kuendekeza malumbano ya kisiasa, na kukatazana kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo si tu kunawachelewesha wao wenyewe katika kujiletea maendeleo yao kwa kasi, lakini wataachwa nyuma na Watanzania wenzao katika maeneo mengine ya nchi.

Rais pia aligawa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya sh milioni 51 ambavyo vilitolewa na na Japan kupitia mfuko wake wa Maendeleo ya Jamii ( JSDF). Vikundi sita kati ya hivyo ni vya akina mama wanaojishughulisha na biashara ya kukaanga samaki na kazi za migahawa, na vilivyobaki ni vya uvuvi, kilimo cha miwa, na ukaushaji/uhifadhi wa samaki.

Vifaa vilivyotolewa kwa vikundi hivyo ni injini saba za kupachika, nyavu 14 za kuvulia, masanduku 102 ya kuhifadhia samaki, friji (deep freezer) kubwa mbili, friji ndogo, vikaango vikubwa vitatu vya kukaangia samaki, meza nne za kuchakatia samaki, viti 14, makasha 152, oven moja ya mkaa.

Katika hatua nyingine, Kikwete amewataka wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri, kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo imelenga katika kuwainua wananchi kimaisha na kuwaongezea kipato.

Rais alisema haipendezi na wala haifurahishi pale mkuu wa mkoa au wa wilaya na hata mkurugenzi anaposhindwa kujua nini kinachofanyika katika eneo lake kuwasaidia wananchi wake ili wajipatie maisha bora.

“Hivi kwa nini mnababaika pale ninapowauliza, niambieni ni miradi gani mnayoitekeleza ya kuwaondolea umaskini wananchi, iwe mmoja mmoja au katika vikundi mnababaika, yaani mnasoma tu kilichoandikwa kwenye taarifa zenu, lakini nikihoji tu basi mnachanganyikiwa tu, acheni kutoa taarifa za kwenye makaratasi, miradi inayohusu wananchi lazima muifahamu kwa kichwa,” alisema rais.

Kauli hiyo ya rais ilifuatia baada ya Mkuu wa Wilaya ya Mafia kushindwa kubainisha kwa uwazi ni miradi gani ambayo wameiandaa kwa ajili ya wananchi wake, hata alipoulizwa mkurugenzi wa halmashauri naye alibabaika, mpaka pale Mbunge wa Jimbo la Mafia, Abdulkarim Shahah, alipojaribu kufafanua.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  3. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Nitaendelea kugombea nafasi za kisiasa- Balozi Karume
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Nthelezi Nesaa
  4. Linda Garner
  5. Marshy Abdu
  6. Prosper Kwigize
  7. Salehe Mmoro
  8. Ramadhan Semtawa
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.