Wito umetolewa kwa serikali na watu binafsi kuwawezesha vijana kujimudu kimaisha ili kuwaepusha na vishawishi vya kijamii ambavyo vitawapelekea kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi
Mheshimiwa Hamis Chubwa, Diwani wa kata ya Muhunga, Kasulu
Wito huo umetolewa na Diwani wa Kata ta Muhunga wilayani Kasulu Bw. Hamis Chubwa wakai akihojiwa na Kigoma yetu juu ya vyanza vinavyochangia kuwepo kwa maambukizi mapya ya virusi vya UKimwi wilayani Kasulu.
Bw. Chubwa amebainisha kuwa kuwepo kwa vijana wanaoshinda vijiweni na katika viambaza vya maduka ya watu wengine bila wao kuingiza chohote pamoja na kupenda starehe za Muziki na sinema ni ishara ya vijana hao kukosa mwelekeo wa kimaisha.
Ametaja kuwa, tabia ya vijana hao kupenda maisha ya hali ya juu bila nyezo kumepelekea kuibuka kwa vijiwe vingi katika maeneo ya masoko ya vijiji na katika barabara kuu ambapo vijana hujadili masuala yasiyo na tija kwao na kutafuta wapenzi.
Aidha amewataka wazazi kuwawekea misingi mizuri ya maisha vijana wao ili wawe na uwezo wa kukabiliana na changamoto za maisha pindi wanapomaliza elimu ya msingi, sekondari na vyuo badala ya kujiingiza katika makubdi ya uharifu na vitendo vya ngono.
Hata hivyo Bw. Chubwa amewataka vijana nao kujitokeza na kujiunga katika vikundi vya akiba na mikopo ambamo anasema wataweza kupata mikopo kutokana na miradi watakayoibua na hatimae kutokomeza utegemezi.
Amewataka pia wanafunzi nao kujibidisha katika masomo yao na kuepuka vitendo vya ngono na kwamba kufanya ngono kwa mwanafunzi huchangia kukwama kimasomo lakini pia kujiongezea nafasi ya kuambukizwa virusi vya ukimwi.
Diwani huyo ambaye licha ya kuwa mwanasiasa, amekuwa akijishughulisha na biashara, pia amewataka wananchi kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu sambamba na kujibidisha katika kazi na michezo kuliko kung’ang’ania anasa za duniani.
Amewataka pia wakazi wa wilaya ya Kasulu kujitokeza kutoa michango ya ujenzi wa mabweni kwa ajili ya wasichana katika shule za sekondari na kuongeza kuwa kundi la wasichana ndilo hasa huathirika na tabia mbaya wawapo shuleni.