Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Jamii  »  Wati 160wakutwa na virusi vya UKIMWI
Wati 160wakutwa na virusi vya UKIMWI
By Prosper Kwigize | Published  11/16/2007 | Jamii | Unrated
Jumla ya watu 160 kati ya watu hamsini na moja elfu na mia tisa themanini na wawili (51982) waliojitokeza kupima virusi vya ukimwi katika tarafa za Heru chini, Manyovu na Makere wilayani Kasulu mkoani Kigoma walikutwa wameambukizwa virusi vya ugonjwa huo.
 
 Hayo yamebainishwa na Mratibu wa kudhibiti Ukimwi wilaya ya Kasulu Dr. Wagwene B. Wagwene wakati akitoa taarifa ya zoezi hilo kwa gazeti la Kigoma Yetu lililotaka kujua mwamko wa wananchi wa jimbo la Magharibi katika kupima virusi vya Ukimwi na namna wanavyopambana na maambukizi mapya.
 
 Imeelezwa kuwa jumla ya watu elfu kumi mia saba ishirini na tisa (17026) wamejitokeza kupima virusi vya ukimwi katika tarafa ya Manyovu katika zoezi la kampeni ya kupima virusi vya ukimwi kitaifa linaloendelea nchini.
 
 Dr. Wagwene alisema katika zoezi hilo jumla ya watu hamsini na tisa (56) wakiwemo wanawake ishirini na nne (24) na wanaume therasini na tano (35) walikutwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
 
 Aidha alibainisha kuwa katika tarafa ya Makere watu elfu saba mia tisa na mbili (7602) walijitokeza kupima afya zao ambapo watu therasini na mbili (32) wakiwemo wanaume kumi na tatu (13) na wanawake kumi na tisa (16) walikutwa na maambukizi ya virusi vya ukumwi.
 
 Dr. Wagwene alisema kuwa jumla ya watu ishirini na saba mia tatu hamsini na nne elfu (27,354) walipima afya zao katika tarafa ya Heru chini wilayani Kasulu na kuvuka lengo lililotarajiwala kupima watu ishirini na moja elfu mia nne ishirini na nane (21428) katikatarafa hiyo.
 
 Katika tarafa ya Heru Chini jumla ya watu 72, wanaume ishirini na wawili (22) na wananwake hamsini (50) walikuwa na wameambukizwa virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Ukimwi.
 
 Zoezi hilo la kampeni ya kupima virusi vya ukimwi kitaifa lililozinduliwa rasimi na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete linaendelea katika wilaya ya kasulu ambapo kwa sasa liko katika tarafa ya Muyama.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  3. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Nitaendelea kugombea nafasi za kisiasa- Balozi Karume
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Nthelezi Nesaa
  4. Linda Garner
  5. Marshy Abdu
  6. Prosper Kwigize
  7. Salehe Mmoro
  8. Ramadhan Semtawa
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.