Habari Tanzania - http://www.habaritanzania.com
Dereva mbaroni kwa kugonga na kuua mara mbili
http://www.habaritanzania.com/articles/4230/1/Dereva-mbaroni-kwa-kugonga-na-kuua-mara-mbili
By Prosper Kwigize
Published on 11/16/2007
 
Dreva wa gari la abiria linalofanya safari zake kati ya Kigoma na Kasulu mkoani Kigoma amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Kasulu mwishoni mwa wiki kwa kosa la kukiuka sheria za usalama barabarani na kusababisha kifo.

· Aliwahi kuua 2005 hakufikishwa mahakamani
 
 Dreva wa gari la abiria linalofanya safari zake kati ya Kigoma na Kasulu mkoani Kigoma amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Kasulu mwishoni mwa wiki kwa kosa la kukiuka sheria za usalama barabarani na kusababisha kifo.
 
 Mwendesha mashtaka wa polisi wilayani Kasulu Bw. Rustis Masota amemtaja dreva huyo kuwa ni ramadhan Ahmad mkazi wa Mwanga Mjini Kigoma na kwamba alimgonga na kumuua Bw. Mohdin Ibrahim.
 
 Imeelezwa mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo tarehe 6 September katika eneo la kijiji cha Kasangezi wilayani Kasulu na kwamba chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi.
 
 Aidha taarifa kutoka jeshi la polisi ambazo zilifikishwa katika mahakama ya wilaya mbele ya hakimu Patrich Ang’ulo zinadai kuwa hilo ni kosa la pili kwa mtuhumiwa huyo ambaye mwaka 2005 aligonga na kuua.
 
 Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyoambatanishwa na kesi mpya, mshtakiwa Ramadhani alimgonga na kumsababishia kifo Bw. Paschal Kimai mkazi wa kijiji cha Nyumbigwa wilayani humo.
 
 Inadaiwa kuwa mtuhumiwa akiendesha gari lenye namba T 644 AJN mali ya Halfan Soud alikuwa akiendesha kwa mwendo kasi na kumgonga marehemu huyo aliyekuwa akitembea kwa miguu.
 
 Hata hivyo mshtakiwa licha ya kushikiriwa na jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani wilayani Kasulu hakufikishwa mahakamani kujibu mashtaka hadi alipokutwa na kosa la pili la September 6 mwaka huu.