Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wapinzani kuipeleka NEC kortini
Wapinzani kuipeleka NEC kortini
By Marshy Abdu | Published  10/3/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
Wapinzani kuipeleka NEC kortini
na Irene Mark


UMOJA wa vyama vinne vya siasa nchini kesho unatarajia kufungua kesi ya kikatiba dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa madiwani nchini.

Katika kesi hiyo itakayosimamiwa na Kampuni ya Uwakili ya Mpoki, inadaiwa kuwa uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba 28, unakiuka haki ya msingi kwa baadhi ya raia kushindwa kupiga kura.

Vyama vitakavyofungua kesi hiyo ni Chama cha Wananchi (CUF), Tanzania Labour Party (TLP), NCCR-Mageuzi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kwa niaba ya wenyeviti wa vyama hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Wilfred Lwakatare, alisema kwamba madhumuni ya kufungua kesi hiyo ni kuitaka mahakama isimamishe uteuzi, kampeni na uchaguzi wa madiwani hao hadi NEC itakapofanya marekebisho kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

Lwakatare alisema kwamba kwa mara ya mwisho wananchi waliandikishwa katika daftari hilo mwaka 2005, hivyo upo uwezekano kwa waliopoteza shahada za kupigia kura, kufariki dunia, kufungwa gerezani au kuhama eneo na kutopiga kura.

“Inawezekana kabisa kuwa waliokuwa na umri wa chini ya miaka 18 walinyimwa kujiandikisha, lakini sasa wamekua wanayo sifa ya kuchagua mwakilishi…hawa hawatapiga kura kwa sababu majina yao hayapo kwenye daftari hilo.

“Hata kwa wale waliokufa, waliofungwa jela, waliohama na kuhamia maeneo yatakayofanyika uchaguzi na waliopoteza shahada watakosa haki yao ya msingi ya kupiga kura,” alisema Lwakatare.

Aidha, naibu katibu mkuu huyo alihoji sababu za Tume ya Uchaguzi kushindwa kuhakiki upya - kwa lengo la kuongeza na kupunguza watu kwenye daftari hilo - kusifanyike kabla ya uchaguzi huo.

Alisema kwamba ikiwa Tume ya Uchaguzi itawaruhusu wagombea wa udiwani kuendelea na kampeni, umoja huo utatoa tamko na kuchukua hatua kali.

Jana, Tume ya Uchaguzi ilikuwa ikitoa fomu za kugombea nafasi ya udiwani kwa wagombea wa kata 16 tofauti zisizokuwa na wakilishi kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo kujiengua uanachama, kufariki dunia na kuachishwa udiwani.

Kata zitakazochagua madiwani na mikoa yake kwenye mabano ni Kilema Kaskazini (Kilimanjaro), Marumba, Majengo na Muhuwesi (Ruvuma), Ifunda na Ulanda (Iringa) na Masuguru (Tanga).

Nyingine ni Mkula na Mwandu (Mwanza), Sombetini (Arusha), Katazi, Namanyere na Kabwe (Rukwa), Namkukwe (Mbeya), Ngulinguli (Shinyanga) na Lipumburu (Mtwara).

Aidha, kampeni za uchaguzi huo mdogo kwa kata zote umeanza rasmi leo na utaendelea hadi Oktoba 27 mwaka huu, siku moja kabla ya uchaguzi kufanyika.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by TN)
    Rating
    excellent - the only coverage to list the wards!
    Kata zitakazochagua madiwani na mikoa yake kwenye mabano ni Kilema Kaskazini (Kilimanjaro), Marumba, Majengo na Muhuwesi (Ruvuma), Ifunda na Ulanda (Iringa) na Masuguru (Tanga).

    Nyingine ni Mkula na Mwandu (Mwanza), Sombetini (Arusha), Katazi, Namanyere na Kabwe (Rukwa), Namkukwe (Mbeya), Ngulinguli (Shinyanga) na Lipumburu (Mtwara).
     
Submit Comment


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.