Habari Tanzania - http://www.habaritanzania.com
Wasomi hawawi nepi.
http://www.habaritanzania.com/articles/4192/1/Wasomi-hawawi-nepi.
By Nthelezi Nesaa
Published on 09/28/2007
 
Wakati wa kudai uhuru, nchi yetu ilipata taabu sana kutokana na mfumo uliokuwa umewekwa na wakoloni. Wakoloni walipoivamia na kuikalia Afrika, walitumia mbinu nyingi chafu kuhakikisha wanaendelea kuinyonya.

Wakati wa kudai uhuru, nchi yetu ilipata taabu sana kutokana na mfumo uliokuwa umewekwa na wakoloni. Wakoloni walipoivamia na kuikalia Afrika, walitumia mbinu nyingi chafu kuhakikisha wanaendelea kuinyonya.
 
 Mojawapo mbinu kati ya nyingi chafu waliyotumia wakoloni ni kuleta wahindi na kuwafanya watu wa daraja la pili huku la kwanza wakiwa wao wazungu na la mwisho waafrika.
 
 Wahindi waliletwa kuwezesha na kurahisisha unyonyaji wa mwafrika huku wakizidisha ugumu wa maisha kwake. Mwafrika aliruhusiwa kulima na kuzalisha mazao yake ya chakula na kulazimishwa kulima mazao ya kikoloni kama vile kahawa, katani,pamba,pareto,chai na mengine mengi kutegemea na mahali alipokuwa.
 
 Baada ya kuvuna mazao yake, hakuruhusiwa kuwauzia wazungu. Hapa ndipo hujuma na uzandiki wa wahindi ulipochimbuka. Kwani kwa kushirikiana na wazungu walihakikisha wanawanyonya waafrika kwa kuwapa bei hafifu na kuwaibia hata kwenye mizani.
 
 Wahandi kama kupe, kupata ulaji wa kirahisi walianza kualikana kiasi cha kujaa barani kwetu hadi leo hii. Kutokana na kupewa mbinu hizi tokana na kujikomba na kujipendekeza kwao kwa mabwana zao wakoloni, walifanikiwa kuendelea kutumia mbinu hizi chafu hadi leo baada ya Afrika kupata uhuru wa bendera ambapo hakika watawala hawakuwa na tofauti na wakoloni katika nchi nyingi ukiachia rangi tu.
 
 Hapa ndipo balaa linaloendelea la kila ufisadi kuwa ndoa baina ya watawala na wafanyabiashara wa kihindi. Hii ni historia. Pia ifahamike katika kudai uhuru walikuwapo baadhi ya wahindi ambao hawakuingizwa kwenye mfumo huu wa kinyonyaji kiasi cha kujikuta upande wa waafrika wakipigania uhuru.
 Mada ya leo ni kutaka kujadili tabaka la wasomi ambao wameamua kujigeuza nepi ili kukidhi matakwa yao ambayo si kingine bali tumbo, njaa, tamaa na ujinga.
 
 Baada ya kuingia siasa za vyama vingi nchini kwetu, kumekuwa na mikakati ya wapinzani kutaka kuchukua dola. Kadhalika na chama tawala kimekuwa na mikakati mingi michafu kama yaliyotokea Arusha hivi karibuni na yaliyokuwa yakijirudia Zanzibar kila uchaguzi, kutoyaachia madaraka.
 
 Kama wakoloni, chama tawala kimebuni aina mpya ya wasaliti. Kipindi hiki siyo wahindi kama wakati wa mkoloni. Kimepata wasomi wa bahati mbaya (Accidental academicians) ambao kama kapu wako tayari kubeba kila aina ya uchafu ilmradi watimize tamaa na njaa zao hata kama ni kwa kujidhalilisha na kuusaliti umma.
 
 Katika kundi hili wamo hata wengine vihiyo ambao hawana jinsi bali kuganga njaa kwa kila namna hata kama ni kwa kutenda jinai kwa vizazi vyao wenyewe. Kama fisi wanakula chochote mradi liende.
 
 Hapa ndipo vyombo vya habari vimevamiwa na mabwana sifa wapendao kuimba kila utukufu wa bwana hata kama haupo! Wengine maskini ni wasomi tena wenye shahada za udaktari! Kama wanasiasa malaya ambao kucha kutwa wanawinda riziki kwa kuhama vyama, nao kadhalika wanadandia kila chombo cha habari chenye jina ili wahanikize sauti zao bwana mkubwa awatupie makombo.
 
 Kwa wasomaji wazuri wa magazeti ya nchini mwetu ni mashahidi kuona watu waliokuwa wakiikosoa serikali ghafla wanageuka kuwa wanaoisifia hata kwa utumbo! Huu ndiyo uchangudoa wa kitaaluma ambapo muhusika usaliti taaluma yake ili aweza kuishi. Huku ndiyo kutumia utumbo kufikiri badala ya ubongo. Huu ndiyo unepi na ukokoro hata umlikwama.
 
 Wapo tena wengi ambao waliwahi kuwa hata na nafasi kiasi cha kuwa na vyombo vyao vya habari lakini bahati mbaya wakiviuza na kujiuza baada ya kushindwa kuvisimamia na kuviendesha. Ni watumwa wa hiari na tumbo ambao kwao riziki haiji ila kwa kutenda jinai.
 
 Kuna usemi kuwa usomi haundoi upumbavu wa mtu. Usemi huu ni kweli kabisa. Kwani ukienda hata kwenye nchi zinazojiita zimeendelea, si ajabu kukuta mtu ana shahada ya udaktari lakini bado akawa shoga au hata msagaji. Je huyu kweli ni msomi au ni mjinga hata mpumbavu? Huyu huenda anaweza kuwa mgonjwa au na matatizo ya homoni.
 
 Lakini inapokuja kwa hawa vyura wapendao kuimba sifa za bwana zisizokuwepo kama ni ugonjwa basi unaweza kuuita tamaasis ufinyuosis ulafitum.
 
 
 Safu hii haitawataja majina. Maana hawakawii kwenda kwa mabwana zao ambao nao watawapa kila msaada kwenda mahakamani ili wakifilisi chombo cha habari ambacho kimewapiga teke kwa kuwastukia. Viumbe hawa laanifu wanakwamisha maendeleo na mstakabali wetu. Hawa fisi kama vibaka ni wa kuchoma moto.
 
 Maana utashangaa mtu anasifia kwa mfano utumbo unaoendelea kutamalaki ambapo mali za nchi zinafujwa na wezi wa chache na familia zao! Inasikitisha na kuchukiza hakuna mfano. Hawa nao ni wahujumu wa taifa hata kama wamewekwa kinyumba na mabwana zao wenye nia mbaya kwa taifa. Hawa midomo chuchungi wanaoitumia vibaya taaluma na kalamu kupata riziki makombo huku wakiukwamisha umma nao ni aina mpya ya majambazi wa kalamu.
 
 Wapo wanajijua na kujulikana. Ni wanafiki ambao hata wanayemtumikia hawampendi bali kama changudoa yeyote wanalazimika ili waishi. Hawa ni watu walioishiwa kimkakati. Maana kwa asili ni uasi unaolenga kuikomboa jamii toka kwenye kila mikatale iwe ya wakoloni weupe au weusi. Usomi siyo udodoki bali u-taa. Usomi ni nyenzo siyo kikwazo cha ukombozi wa kweli wa jamii. Msomi anayeangalia maslahi yake peke yake amefilisika na amepata elimu anayoifuja kwa makosa kabisa.
 
 Hapa Tanzania kuna wasomi wa kupigiwa mfano kama Profesa Issa Shivji ambaye bila kujali maguvu ya serikali wala chochote huwa akipata nafasi anaiambia kavu kavu. Juzi juzi kwa mfano alisema watanzania wanaishi kama watumwa ilhali waliahidiwa kupelekwa Kanani.
 
 Maneno yake hayakuwafurahisha watawala. Naye alijua fika kuwa yatawaudhi. Maana wamezoea kusifiwa hata wasipostahili wasijue kutegemea nyimbo za vyura na vyangudoa ni kujidanganya na isitoshe nayo ni dalili ya kufilisika kulihali.
 
 Wasomi uchwara hawa kwa kuchanganyika na matapeli wa kawaida wa uandishi maarufu kama kanjanja wamepenyezwa karibu kila gazeti ili kutapakaza sumu yao. Ni vizuri kuwataarifu wasomaji kuwa kuna kundi hili chafu na fisidi linaloshangilia maangamizi ya jamii.
 
 Leo ukisikia kwa mfano mtu analisifia bunge kwa kumfukuza mwakilishi wa umma kwa kutimiza wajibu wake kwa waliomchagua na kumtuma dhidi ya wezi wachache wanaojificha nyuma ya pazia la utukufu, mhukumu moja kwa moja kuwa huyu ameishiwa na hafai kuitwa msomi. Ukimuita msomi basi si mwingine bali msomi nepi ambaye anaweza kutumiwa na kila mwenye kichanga chake kufunika haja za kichanga hata mtoto mkubwa tu.
 
 Hawa wakichanganyikana na wanasiasa mbwa mwitu na mafisi, ujue nchi ina kazi nzito ya kuwaandama na kuwasuta ili wakome kufikiria kwa kutumia utumbo badala ya ubongo. Hawa nao wamekosa maadili sawa na vyangudoa wa kawaida pale mitaa ya Ohio. Hawa na wale majambazi waliopigwa risasi pale Moshi hawana tofauti kwani wote ni watenda jinai.
 
 Hawa wanaojitia kwenye utumwa wa hiari si watu wa kuonea aibu wala kuwakabili kwa lugha ya kistaarabu. Utawakabilije kistaarabu wakati wanachofanya ni kitendo kisichopaswa kutendwa na binadamu?
 
 Kuna haja ya vyombo vya habari visivyokuwa nyumba ndogo ya serikali kutoa safu maalumu ya kuwawezesha wasomaji kutoa duku duku zao kuhusiana na matapeli hawa wa kalamu ambao nao kimsingi hawana tofauti na wezi wengine wa kalamu kama tunaoshuhudia baada ya kuanza kwa siasa za kijambazi,kinafiki,kirafiki, na kisanii.
 nesaa@yahoo.com