Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mahakama yaamru Mrema akamatwe
Mahakama yaamru Mrema akamatwe
By Marshy Abdu | Published  09/19/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
Mahakama yaamru Mrema akamatwe
na Nuru Yanga


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jana ilitoa hati ya kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) Augustine Mrema na wenzake watatu.

Amri hiyo inakuja wakati Mrema akiwa miongoni mwa viongozi wa vyama vinne vya upinzani wanaozunguka katika mikoa mbalimbali hapa nchini wakiwahamasisha wananchi kukikataa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao, wakiwatuhumu viongozi wake kujihusisha na vitendo vya rushwa na kuhujumu rasilimali za nchi.

Watu hao wanatakiwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani hapo kutokana na tuhuma za kushindwa kuhudhuria katika kesi yao ya uchochezi, ambayo imefunguliwa katika mahakama hiyo.

Akiomba hati hiyo jana, Mwendesha Mashitaka, Inspekta wa Polisi, Pamphil Mhollery, alidai mbele ya Hakimu Said Msuya, kuwa imekuwa ni kawaida kwa washitakiwa hao kutokuhudhuria mahakamani hapo bila kutoa sababu zozote za msingi.

Katika kesi hiyo ya mwaka 2002, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, Mrema na wenzake walitoa maneno ya uchochezi dhidi ya serikali, wakidai kuwa wachimbaji wadogo wadogo wa eneo la Bulyanhulu wilayani Kahama, katika Mkoa wa Shinyanga, walifukiwa wakiwa hai.

Watuhumiwa hao walidai katika maelezo yao kuwa, wachimbaji hao walipatwa na vifo hivyo, katika harakati za kuwaondoa kwa nguvu, baada ya eneo hilo kuuzwa kwa mwekezaji kutoka nje ya nchi.

Ili kuthibitisha kuwa serikali ilikuwa na nia ovu dhidi ya wachimbaji hao, Mrema na wenzake wanadaiwa kusema kuwa baada ya kuwafukia wakiwa hai, hata baada ya madai hayo kutolewa na wanaharakati, serikali haikuchukua hatua zozote.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, Mrema na wenzake walitoa maneno hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mwaka 2002 katika viwanja vya Manzese, Argentina jijini Dar es Salaam.

Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, alikubali kutolewa kwa hati hiyo na kuipangia kesi hiyo iendelee tena Oktoba 19 mwaka huu mara baada ya kukamatwa kwa washitakiwa.

Kati kesi nyingine, mhasibu katika Ubalozi wa Afrika Kusini nchini, Makole Kusekwa (34) alifikishwa katika mahakama hiyo akikabiliwa na tuhuma za kula njama na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kiasi cha sh milioni nane mali ya ubalozi huo.

Makole alijipatia fedha hizo kwa kughushi saini ya Ntombe Lungisani, ambaye ni ofisa utawala katika ubalozi huo, katika hati kadhaa za miezi tofauti ambazo zinaonyesha kuwa zimetolewa kihalali.

Awali, ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka Maxwiliam Biligi, kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo kati ya Januari 23 na Agosti 24 mwaka huu.

Hata hivyo, mshitakiwa alikana kosa hilo na yuko nje kwa dhamana hadi kesi yake itakapotajwa tena Oktoba 3, mwaka huu.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.