Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Walemave wilayani Kasulu wapatiwa msaada wa baiskeli.
Walemave wilayani Kasulu wapatiwa msaada wa baiskeli.
By Prosper Kwigize | Published  09/4/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:

Shirika la msaada wa injili vijijini lenye makao makuu jijini Dar es salaam limetoa msaada wa baiskeli tano kwa walemavu wilayani kasulu mkoani kigoma.

Msaada huo ulikabidhiwa na afisa mtendaji wa kijiji cha Murubona Bw.Thomas Magambo kwa niaba ya mkurugenzi mtrendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu, katika hafla ndogo iliyofanyika katika ukumbi wa standi mpya ya mabasi mjini Kasulu.

Mkurugenzi wa shirika hilo Bw.Borakupata Ndunguru akitoa maenlezo ya msaada huo maalumu alisema, msaada huo umetolewa na shirika hilo baada ya kupata maombi kutoka kwao na kwa wazazi wao baada ya kupata ushauri kutoka kwa mwakilishi mkazi wa taasisi hiyo wilayani Kasulu.

Alibainisha kuwa taasisi yake ya kidini ilipokea maombi matano kutoka wilayani Kasulu na kwamba baiskeli moja iligawiwa kwa mlemavu mmoja wa mjini Kigoma baada ya kupatikana kwa taarifa kuwa mlemavu wmmoja wa Kasulu alikwisha pata baiskeli.

Aidha Bw. Ndunguru aliwataka waumini wa madhehebu mbalimbali kubuni mbinu za kutoa misaada kwa walemavu bila kutegemea watu kutoka nje ya wilaya zao au nje ya nchi.

Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa wadau mbalimbali pamoja na serikali kutowabagua walemavu na kutojinufaisha na misaada ya watu walio katika makundi maalumu hususani walemavu, wajane na waathirika wa virusi vya ukimwi.

Alibainisha kuwepo kwa baadhi ya taasisi za umma na binafsi ambazo huomba misada nje ya nchi au hata serikalini na kasha kujinufaisha kwa manufaa yao na kuwadhurumu walengwa wa misaada hiyo

Shirika la msaada wa injili vijijini lenye makao makuu yake jijini dar es salaam lilianzishwa na wainjilist mbalimbali miaka mitatu iliyopita kwa nia ya kutoa elimu ya injili na misaada ya kiutu vijijini.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.