Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  REDESO lamjengea nyumba mzee aliyetelekezwa
REDESO lamjengea nyumba mzee aliyetelekezwa
By Prosper Kwigize | Published  01/1/1970 | Habari za Kitaifa | Rating:
Kibondo
Shirika la mazingira na haki za binadamu la REDESO wilayani Kibondo limetoa msaada wa ujenzi wa nyumba kwa mzee mmoja aliyetelekezwa na mwanae na kumwacha bila makazi.
 
 Mwanasheria katika shirika la Redeso ambaye pia ni msimamizi wa Kituo cha sheria na utetezi wa kijinsia katika kituo cha Rusohoko Bi Edna Kamareki amemtaja mzee huyo kuwa ni Gabliel Ruvako mwenye umri wa miaka 90 mkazi wa kijiji cha Rusohoko.
 
 Amesema katika kutoa huduma kwa wananchi wa kijiji hicho Redeso ilimbaini mwananmke mmoja ambaye ni mkamwana wa mzee Ruvako ambaye naye alitelekezwa na mzee huyo.
 
 Bi. Kamareki ameeleza kuwa wakati wakifikiria kumtetea mama huyo aliyemtaja kwa jina la Advela Benector walibaini kuwa anaishi na mzee Ruvako kwenye nyumba iliyobomoka.
 
 Amebainisha kuwa shirika hilo liliamua kuwashawishi wananchi kupitia kwa viongozi wa mtaa ili kumjengea nyumba mzee huyo ambayo hadi sasa imekamilika msingi na ujenzi wa ukuta umeanza.
 
 Aidha Bi. Kamareki aameeleza kuwa jingo hilo litagharimu zaidi ya kiasi cha pesa tasilimu shilingi 71 elfu pamoja na michango ya nguvu kazi ya wananchi na usafirishaji wa zana za ujenzi utakao fanywa na REDESO.
 
 Hii ni mara ya Kwanza kwa shirika la REDESO kuamua kumjengea nyumba mwananchi mwenye shida iliyotokana na kutelekezwa na familia yake.
 

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  3. Is Tanzania a safe place to invest?
  4. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
  5. Nitaendelea kugombea nafasi za kisiasa- Balozi Karume
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Linda Garner
  4. Nthelezi Nesaa
  5. Marshy Abdu
  6. Prosper Kwigize
  7. Salehe Mmoro
  8. Ramadhan Semtawa
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.