Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Msafara wa Vuai wajeruhi mwanafunzi
Msafara wa Vuai wajeruhi mwanafunzi
By Habari Tanzania | Published  08/26/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
MSAFARA wa Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, umemgonga mwanafunzi mmoja wa shule ya Sekondari ya Mission na kusababisha kuvunjika mkono.

Mwanafunzi aliyepatwa na mkasa huo ni farida Mhagama, ambaye anasoma kidato cha pili katika shule hiyo.

Hali hiyo ilitokea eneo la Mfaranyaki karibu na kituo cha mafuta cha Kisumapei, wakati msafara wa Vuai ukitokea Mbinga kuelelekea Manispaa ya Songea.

Ajali hiyo ilihusisha gari la polisi la Kituo cha Namtumbo, lenye namba PT 0833.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa, Benedict Ngaiza, alithibitisha hospitali hiyo kumpokea mwanafunzi huyo ambaye wamemfunga POP na kumpatia dawa za kupunguza maumivu.

Kaimu mkuu wa mkoa ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Gabriel Kimolo, aliyekuwepo katika msafara huo alifika hospitalini hapo kumpa pole mwanafunzi huyo na kuahidi kumgharamia matibabu.

Vuai yuko mkoani Ruvuma kwa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kwamba wakati ajali hiyo inatokea alikuwa akitokea kuzindua msikiti eneo la Litumbandesi.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.