Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Hujuma hizi katika kata ya MINEPA zitakwisha lini
Hujuma hizi katika kata ya MINEPA zitakwisha lini
By Habari Tanzania | Published  08/21/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mungu ambae ametupa uzima.
Napenda pia kuwashukuru viongozi wetu wa chama na serikali kwa jinsi wanavyowajibika katika kuwatumikia watanzania katika wilaya hii ya Ulanga.
 
Napenda kutoa masikitiko yangu kwenu ninyi viongozi wetu kwa yale yanayotusibu sisi wananchi wenu tuliowapa dhamana ya kutuongoza. Inawezekana hamfahamu yale yanayotokea katika kata yetu ya Minepa, lakini kwa uchungu mkubwa napenda kusema matendo ya baadhi ya viongozi wa kata yetu yanahujumu uchumi wa taifa letu na haki za binaadam.
 
kwanza kabisa viongozi wa kata hii  hawataki kushughuikia matatizo ya wananchi mpaka wamepewa hela, kwa mfano kuna kesi ya mama mmoja wa kisukuma alibakwa akaambiwa ili swala lake lishughulikiwe inabidi atoe sh 50000.sasa hii ni haki kweli jamani?
 
Mungu pia ametubariki na swala la  kilimo cha umwagiliaji lakini watu wa kamati ya maji wamekuwa kama miungu , wananyanyasa wengine na kuwafanya wasitumie maji aliyotupa Mungu kwa uhuru, mimi nasema hizo ni hujuma katika kampeni za rais za kuleta mapinduzi ya kilimo. Nauliza jamani kwa nini watu wachache waiweke serikali ya kata mfukoni , na wananchi wasitendewe haki.kila mtanzania anayo haki ya kulima na kutmia maji ambayo MUNGU AMETUPA BURE. Ombi langu kwa mkuu wa wilaya, viongozi hawa hawatufai,  waonywe, tunomba pia takuru ifike vijijin ili tupewe haki.
 
kwa leo naomba niishie hapo
Mungu ibariki Tanzania ,mungu ibariki kata ya Minepa.
Ni mimi mwanachi mpenda maendeleo

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.