Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Serikali yaibiwa mafuta
Serikali yaibiwa mafuta
By Habari Tanzania | Published  08/19/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Mwandishi Wetu


SERIKALI inaibiwa maelfu ya lita za mafuta ya petroli na dizeli na watumishi wake.

Uchunguzi wa muda mrefu wa Tanzania Daima Jumapili, umebaini kuwa wafanyakazi wanaohusika na wizi huo ni baadhi ya madereva wa magari ya serikali na wafanyakazi wa visima vya mafuta vya serikali.

Watumishi wanaohusika na wizi huo wamebainika kuwa na ukwasi wa kutisha wakiwa wanamiliki nyumba na magari ya kifahari sehemu mbalimbali za nchi.

Uchunguzi umebaini kuwa mbinu kubwa inayotumiwa kuiba mafuta hayo ni kudanganywa maofisa wanaohusika na kuidhinisha kutolewa kwa mafuta hayo kupelekwa katika visima vya serikali.

Watumishi katika visiwa hivyo huongopa kwa wakubwa wao kuhusu akiba ya mafuta iliyo katika visima na wanapopewa shehena nyingi, iliyosalia katika visiwa hivyo huiuza kwa madereva wa magari ya serikali ambao nao huyauza kwa watu binafsi na baadhi ya wafanyabiashara.

Baadhi ya visima vilivyofanyiwa uchunguzi na gazeti hili na kubainika kuhusika na vitendo hivyo vya wizi ni vile vilivyo katika Wilaya ya Temeke.

Madereva waliobainika kuhusika na vitendo hivyo ni wa wizara mbalimbali za serikali pamoja na taasisi kadhaa zinazohudumiwa mafuta na serikali.

Uchunguzi zaidi umebaini kuwa mafuta yanayoibwa huuzwa katika maeneo ya bandari, Mivinjeni na Keko.

Mmoja wa wafanyakazi wa Wizara ya Fedha aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la jina lake kutoandikwa gazetini alieleza kuwa ni rahisi kuwatambua watumishi wanaohusika katika wizi huo kutokana na mali wanazomiliki ambazo hazilingani hata kidogo na vipato vyao.

“Usifanye mchezo bwana, kwa kweli hawa wenzetu wanakula kuku, pesa wanazozipata kutokana na wizi huo wa mafuta zimewaweka mahali pazuri, wengi ni matajiri.

“Wenzetu wanafaidika, wengi wamejiwekea vitega uchumi vingi huku wakiendelea kuchota pesa lukuki,” alisema.

Uchunguzi unaonyesha kuwa idadi ya mafuta inayoibwa ni kubwa ambapo mtu mmoja huuza kiasi cha lita zaidi ya 50 kwa siku.

Gazeti hili likiwa katika kisima kimoja cha serikali wilayani Temeke lilihakikishiwa na mmoja wa watumishi wa kisima hicho kuwa linaweza kupata kiasi chochote cha mafuta linachokihitaji.

Biashara ya kuuza mafuta ya wizi hufanywa na madereva nyakati za asubuhi na jioni na wanunuzi wakubwa ni madereva wa daladala, teksi na magari binafsi.

Alhamisi wiki hii, gazeti hili liliwasiliana na makao makuu ya Jeshi la Polisi kuhusu tuhuma hizo, msemaji wake, Essaka Mugasa, aliomba kupewa muda hadi Jumamosi kwa ajili ya kulifanyia kazi jambo hilo.

Alipoulizwa tena jana kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu suala hilo alieleza kuwa bado uchunguzi wa suala hilo unaendelea hivyo polisi haiwezi kutoa tamko lolote.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.