Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Uchumi  »  Watuhumiwa wizi NMB Mwanga kizimbani
Watuhumiwa wizi NMB Mwanga kizimbani
By Habari Tanzania | Published  08/16/2007 | Uchumi | Unrated
na Beatrice Maina, Moshi


WAHUTUMIWA 13 wa kesi ya kuvamia na kupora fedha zaidi ya sh milioni 234 katika benki ya NMB tawi la Mwanga, mkoani Kilimanjaro, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi.

Washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Geni Dudu na kusomewa mashitaka manne, likiwemo la mauaji ya askari Michael Milanzi aliyekuwa mlinzi wa benki hiyo.

Mwendesha Mashitaka, Inspekta wa Polisi, Enos Lukyaa, alidai washtakiwa wote wanakabiliwa na mashitaka ya kula njama kwa nia ya kutenda kosa, unyang’anyi wa kutumia silaha, uporaji wa silaha na mauaji.

Akiwasomea mashitaka hayo, alidai kuwa Julai 11 mwaka huu, saa 1.30 jioni, washitakiwa hao walipora sh milioni 234 mali ya benki hiyo pamoja na bunduki mbili na magazine zake zilizokuwa na risasi 60.

Inspekta Lukyaa alidai kuwa, pia washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya askari PC Michael Milanzi.

Aliwataja washitakiwa hao kuwa ni Samwel Gitau Saitoti (30) na Michael Kimani Peter (37) raia wa nchi jirani ya Kenya, Fadhili Msuya (40), askari aliyefukuzwa PC Nathaniel Amon (33), Devotha Elias Msanze (32), Julian Elias Msanze (47), Elizabeth Elias Msanze (28) na Ntibasalila Elias Msanze (18) wote wakazi wa jijini Arusha.

Wengine ni Calist Joseph (44), Deodat Willium Temu (36), Emmanuel Eliaza Mziray (33), Frorian Kimati (39) na Salome Sebastian Matemu (54) ambaye ni meneja operesheni wa benki hiyo, wote wakazi wa maeneo mbalimbali mkoani Kilimanjaro.

Hata hivyo, washitakiwa walikana mashitaka hayo, ila kwa shitaka la mauaji hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo kisheria haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Washitakiwa wamerudishwa rumande hadi Agosti 29 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.

Kesi hiyo inaendeshwa na wakili wa serikali, Peter Maugo na mshitakiwa, Calist Joseph akitetewa na wakili wa kujitegemea, Anzameni Shayo.

Pamoja na watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani, bado Jeshi la Polisi mkoani hapa linawasaka watu wengine sita kuhusiana na tukio hilo la uporaji wa benki hiyo na mauaji hayo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Lucas Ng’hoboko, wanaosakwa ni Gabriel Frank (28) mkazi wa Vatican Sinza jijini Dar es Salaam, Edger William Ndesokia Minja, Aloyce Silvester Shija, mkazi wa Pasua mjini Moshi na Thomas Edward Laizer, mkazi wa Njiro Arusha.

Wengine ni Shehe ambaye anatambulika kwa jina moja, mkazi wa Arusha na Moshi pamoja na kijana maarufu kama Kamwana mkazi wa Arusha.

Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo wakiongozwa na ulinzi mkali, wakiwemo askari wa kutuliza ghasia (FFU), askari kanzu, mbwa, farasi, pikipiki na magari, ambapo pia kulikuwa na umati mkubwa wa mamia ya watu waliofika mahakamani hapo kushuhudia watu hao wakipandishwa kortini.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  3. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Nitaendelea kugombea nafasi za kisiasa- Balozi Karume
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Nthelezi Nesaa
  4. Linda Garner
  5. Marshy Abdu
  6. Prosper Kwigize
  7. Salehe Mmoro
  8. Ramadhan Semtawa
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.