Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kikwete aisifu ufufuaji kahawa mkoani Kilimanjaro
Kikwete aisifu ufufuaji kahawa mkoani Kilimanjaro
By Habari Tanzania | Published  08/6/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Waandishi Wetu, Moshi

RAIS Jakaya Kikwete ameipongeza Kampuni ya Kilimanjaro Plantation kwa kufufua zao la kahawa na kuliagiza Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kutatua tatizo la umeme.

Kikwete alitoa agizo hilo jana mjini hapa baada ya kutembelea shamba la kahawa lenye ukubwa wa hekari 1,530 ambalo zamani lilikuwa likifahamika kama Tchibo Estate na kuridhishwa na ufufuaji wa kahawa.

Agizo la Rais Kikwete lilitokana na taarifa iliyosomwa kwake na Meneja Mradi wa kampuni hiyo, Peter Gethi ambaye alimweleza juu ya umeme kukosa nguvu na kuathiri uzalishaji.

Gethi pia alimweleza Kikwete kuwa, kampuni hiyo inakabiliwa na matatizo mengine kama ya upungufu wa maji kwenye mito na kuongezwa kwa eneo la akiba ya barabara na hivyo kufanya ardhi ya shamba kumegwa.

Tangu ianze kazi ya kufufua kahawa mwaka 2000, kampuni hiyo imewekeza kiasi cha Sh6 Bilioni na sehemu kubwa imeelekezwa kwenye umwagiliaji kwa njia ya matone na mabwawa ya maji.

Alisema tekinolojia ya umwagiliaji kwa njia ya matone, inapunguza matumizi ya maji kwa asilimia 70 ikilinganishwa na vinyunyizio vingine na mifereji ya asili, hivyo kudhibiti upotevu wa maji.

�Njia hii pia inatufanya tuweke mbolea vizuri bila upotevu kwa kuelekeza moja kwa moja kwenye mmea kwa njia ya kuiyeyusha na kuiweka kwenye msukumo wa matone yanaokwenda moja kwa moja kwenye mmea," alisema.

Aliongeza kuwa, kampuni hiyo imekuwa ikishiriki kikamilifu kusaidia miradi ya maendeleo ya jamii ambapo imetoa Sh41.5 milioni kwa ajili ya miradi ya elimu na kugawa bure miche 322,000 ya kahawa.

Baada ya taarifa hiyo, Kikwete alilitaka TANESCO kutatua tatizo la umeme akisema bila nishati hiyo kuwa ya uhakika na yenye nguvu, ukoboaji wa kahawa katika kiwanda cha kampuni hiyo unaweza kukwama.

Kuhusu kumegwa kwa shamba la kampuni hiyo, Rais alimwagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kukutana na uongozi wa kampuni hiyo kuzungumzia hatima ya kulipwa fidia.

Hata hivyo, alisema kuhusu uhaba wa maji, serikali haina ubavu wa kutatua na kuitaka kampuni hiyo, kuendelea kuchimba visima na kuwasaidia wananchi kuboresha vyanzo vya maji.

Kikwete yuko katika ziara ya siku sita mkoani Kilimanjaro, ambako pamoja na mambo mengine, amekuwa akifungua miradi ya maendeleo ikiwamo ya elimu na kuhutubia mikutano ya hadhara.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.