Habari Tanzania - http://www.habaritanzania.com
Nitaendelea kugombea nafasi za kisiasa- Balozi Karume
http://www.habaritanzania.com/articles/408/1/Nitaendelea-kugombea-nafasi-za-kisiasa--Balozi-Karume
By Habari Tanzania
Published on 06/30/2006
 
 
Balozi wa Tanzania aliemaliza muda wake nchini Ujerumani Balozi Ali Karume amesema bado hajakata tamaa katika kutafuta nafasi za kisiasa na anakusudia kuomba tena ridhaa ya wanachama wa CCM katika chaguzi zijazo.

Balozi wa Tanzania aliemaliza muda wake nchini Ujerumani Balozi Ali Karume amesema bado hajakata tamaa katika kutafuta nafasi za kisiasa na anakusudia kuomba tena ridhaa ya wanachama wa CCM katika chaguzi zijazo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake mjini Berlin, Ujerumani Balozi Karume alikiri kuwa aliingia katika kinyang`anyiro cha mwaka jana akijua kabisa kuwa nafasi yake ni ngumu sana alihisi ilibidi kuanza pahala.

``Elimu ninayo,nina digrii tatu nimechukua marekani na nashukuru nimeaminiwa na marais wa awamu zote mbili niliofanya nao kazi wamewahi kuniomba kuchukua nafasi kubwa sana katika nchi yetu lakini nilikataa kwa vile nilidhani muda bado, lakini sasa nadhani baada ya kuwa balozi kwa miaka kumi na nne sasa nimewiva na uwezo ninao hivyo sioni kwa nini nisigombee tena``

Alipoulizwa kuhusu mazingira ya uhamisho wake na iwapo kauli ya Ikulu kuwa 创atapangiwa kazi nyingine创 pengine ni siasa tu kwa vile kishaondolewa Balozi Karume alisema ameichukulia kauli hiyo vizuri kwa vile anadhani Rais kaamua kutafakari nafasi gani itamfaa zaidi baada ya kuwa nje kwa miaka 14.

创Mimi nimeichukulia positively tu kuwa rais kaamua huyu bwana ngoja kwanza nitafakari wapi aende ana uzoefu mkubwa na pia hakuna haraka kwenye mambo haya创. Alipobanwa kuwa haoni kuwa kwa kugombea kwake katika uchaguzi wa mwaka jana ndani ya CCM atakuwa amejiwekea mazingira magumu kuweza kufanya kazi ndani ya serikali ya sasa Balozi Karume alikanusha hilo na kusema kuwa kwa sasa ni vyema kusubiri kazi atakayopangiwa iangaliwe kama ataimudu au la ingawa pia aliweka bayana kuwa si kazi zote anazoweza kukubali.

创Mimi ni mwanadamu bwana mwandishi hufika wakati nikaona kabisa hii kazi niliopangiwa kabisa haiendani na kisomo changu na uwezo wangu na rekodi yangu, na ni wazi kuwa nikipewa kazi ambayo nimeiona hivyo nitamwambia mheshimiwa Rais ndugu yangu ahsante sana nadhani utumishi wangu unakoma hapa niendelee na shughuli zangu创 alisisitiza.

Aidha akizungumzia nafasi yake kisiasa Tanzania Balozi Karume alisema amewahi kuombwa na marais Mwinyi na Mkapa kutumikia taifa katika nafasi kubwa zaidi ya aliyonayo sasa lakini alikataa kuitikia wito huo kwa vile muda wake ilikuwa bado lakini fursa hiyo ikitokea tena hatosita kuichukua. Hata hivyo alipobanwa kufafanua ni kazi gani hiyo aliyopewa na kuikataa Balozi Karume alikataa kusema na kusema muda ukifika itakuwepo katika kitabu cha kuelezee maisha yake pindi akishastaafu.

创Lakini nikwambie tu kuwa mwaka 1988 pale London unapotoka Rais Mwinyi aliniita kuniomba niifanye kazi hiyo lakini nilikataa kwa nia njema kabisa na hata Rais Mkapa katika kipindi cha pili cha uongozi wake aliniambia niifikirie kazi hiyo lakini niliona muda wake bado, lakini bwana mwandishi nakuthibitishia lau fursa hii ikitokea tena nadhani nimewiva na muda tayari nitafanya, nashindwa siwezi kuweka bayana kwa sasa kwa vile nadhani inabidi nihifadhi haya kwa ajili ya biography yangu ili na wenzangu wajue niliwahi kuombwa kazi kubwa创 alisisitiza Balozi Karume.

Akizungumzia juu ya mafanikio ya ubalozi wake nchini Ujerumani alisema anadhani ameongoza vizuri ubalozi hususan katika kipindi cha mpito kuelekea kuhamisha ubalozi kutoka Bonn kuhamia Berlin na pia kuweka mahusiano mazuri na serikali ya shirikisho ya ujerumani na serikali ndogondogo saba kati ya kumi na sita.

创Hakika nadhani katika vitu nitakavyosema naviwacha kama ni changamoto kwa mwenzangu atakaekuja ni kuwa hana budi kuendeleza haya mahusiano manake yamesaidia misaada mingi kupatikana na sina budi kusema sikuweza kuweka mahusiano na serikali ndogo ndogo za majimbo tisa hivyo kama ni kufeli basi labda hii ndio failure yangu创

Hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete aliteua mabalozi kadhaa ambapo Balozi Ngemera aliekuwa katika jumuiya ya Afrika Mashariki kama naibu katibu mkuu anaeshughulikia utawala na fedha aliteuliwa kuchukua nafasi ya balozi Ali Karume ambae taarifa ya Ikulu ilisema atapangiwa kazi nyingine.

Haya ni mahojiano ya kwanza ambayo Balozi Karume amekubali kufanya tangu taarifa ya kuhamishwa kwake ilipotolewa na Ikulu.