Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

Search

Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Nitaendelea kugombea nafasi za kisiasa- Balozi Karume
Nitaendelea kugombea nafasi za kisiasa- Balozi Karume
By Habari Tanzania | Published  06/30/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:

Balozi wa Tanzania aliemaliza muda wake nchini Ujerumani Balozi Ali Karume amesema bado hajakata tamaa katika kutafuta nafasi za kisiasa na anakusudia kuomba tena ridhaa ya wanachama wa CCM katika chaguzi zijazo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake mjini Berlin, Ujerumani Balozi Karume alikiri kuwa aliingia katika kinyang`anyiro cha mwaka jana akijua kabisa kuwa nafasi yake ni ngumu sana alihisi ilibidi kuanza pahala.

``Elimu ninayo,nina digrii tatu nimechukua marekani na nashukuru nimeaminiwa na marais wa awamu zote mbili niliofanya nao kazi wamewahi kuniomba kuchukua nafasi kubwa sana katika nchi yetu lakini nilikataa kwa vile nilidhani muda bado, lakini sasa nadhani baada ya kuwa balozi kwa miaka kumi na nne sasa nimewiva na uwezo ninao hivyo sioni kwa nini nisigombee tena``

Alipoulizwa kuhusu mazingira ya uhamisho wake na iwapo kauli ya Ikulu kuwa ´´atapangiwa kazi nyingine´´ pengine ni siasa tu kwa vile kishaondolewa Balozi Karume alisema ameichukulia kauli hiyo vizuri kwa vile anadhani Rais kaamua kutafakari nafasi gani itamfaa zaidi baada ya kuwa nje kwa miaka 14.

´´Mimi nimeichukulia positively tu kuwa rais kaamua huyu bwana ngoja kwanza nitafakari wapi aende ana uzoefu mkubwa na pia hakuna haraka kwenye mambo haya´´. Alipobanwa kuwa haoni kuwa kwa kugombea kwake katika uchaguzi wa mwaka jana ndani ya CCM atakuwa amejiwekea mazingira magumu kuweza kufanya kazi ndani ya serikali ya sasa Balozi Karume alikanusha hilo na kusema kuwa kwa sasa ni vyema kusubiri kazi atakayopangiwa iangaliwe kama ataimudu au la ingawa pia aliweka bayana kuwa si kazi zote anazoweza kukubali.

´´Mimi ni mwanadamu bwana mwandishi hufika wakati nikaona kabisa hii kazi niliopangiwa kabisa haiendani na kisomo changu na uwezo wangu na rekodi yangu, na ni wazi kuwa nikipewa kazi ambayo nimeiona hivyo nitamwambia mheshimiwa Rais ndugu yangu ahsante sana nadhani utumishi wangu unakoma hapa niendelee na shughuli zangu´´ alisisitiza.

Aidha akizungumzia nafasi yake kisiasa Tanzania Balozi Karume alisema amewahi kuombwa na marais Mwinyi na Mkapa kutumikia taifa katika nafasi kubwa zaidi ya aliyonayo sasa lakini alikataa kuitikia wito huo kwa vile muda wake ilikuwa bado lakini fursa hiyo ikitokea tena hatosita kuichukua. Hata hivyo alipobanwa kufafanua ni kazi gani hiyo aliyopewa na kuikataa Balozi Karume alikataa kusema na kusema muda ukifika itakuwepo katika kitabu cha kuelezee maisha yake pindi akishastaafu.

´´Lakini nikwambie tu kuwa mwaka 1988 pale London unapotoka Rais Mwinyi aliniita kuniomba niifanye kazi hiyo lakini nilikataa kwa nia njema kabisa na hata Rais Mkapa katika kipindi cha pili cha uongozi wake aliniambia niifikirie kazi hiyo lakini niliona muda wake bado, lakini bwana mwandishi nakuthibitishia lau fursa hii ikitokea tena nadhani nimewiva na muda tayari nitafanya, nashindwa siwezi kuweka bayana kwa sasa kwa vile nadhani inabidi nihifadhi haya kwa ajili ya biography yangu ili na wenzangu wajue niliwahi kuombwa kazi kubwa´´ alisisitiza Balozi Karume.

Akizungumzia juu ya mafanikio ya ubalozi wake nchini Ujerumani alisema anadhani ameongoza vizuri ubalozi hususan katika kipindi cha mpito kuelekea kuhamisha ubalozi kutoka Bonn kuhamia Berlin na pia kuweka mahusiano mazuri na serikali ya shirikisho ya ujerumani na serikali ndogondogo saba kati ya kumi na sita.

´´Hakika nadhani katika vitu nitakavyosema naviwacha kama ni changamoto kwa mwenzangu atakaekuja ni kuwa hana budi kuendeleza haya mahusiano manake yamesaidia misaada mingi kupatikana na sina budi kusema sikuweza kuweka mahusiano na serikali ndogo ndogo za majimbo tisa hivyo kama ni kufeli basi labda hii ndio failure yangu´´

Hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete aliteua mabalozi kadhaa ambapo Balozi Ngemera aliekuwa katika jumuiya ya Afrika Mashariki kama naibu katibu mkuu anaeshughulikia utawala na fedha aliteuliwa kuchukua nafasi ya balozi Ali Karume ambae taarifa ya Ikulu ilisema atapangiwa kazi nyingine.

Haya ni mahojiano ya kwanza ambayo Balozi Karume amekubali kufanya tangu taarifa ya kuhamishwa kwake ilipotolewa na Ikulu.
 
How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by FLORA KOMBA)
    Rating
    Balozi amejieleza vizuri jinsi alivyopokea mabadiliko hayo. Kipindi cha miaka 14 kuwa nje ni muda mrefu sana. Akubali kupangiwa kazi nyingine ili aweze kuendelea yale aliyojifunza nje Ujerumani na kuyaleta Tanzania.
     
  • Comment #2 (Posted by abdallah Rajab S Kizae)
    Rating
    Maoni yake ni mazuri inaonyesha amekomaa kwa
    ninavyo mfahamu Ali Karume
     
  • Comment #3 (Posted by hellen)
    Rating
    Kila la kheri. naamini misaada mingi ya ujerumani tanzania ni pamoja na juhudi zako kupitia GTZ.Nimeona wewe ni msomi sana,nina imani bado una nafasina uwezo mkubwa wa kulitumikia taifa hili, kwa wazanzibari ijapokuwa hakuwa na digirii nyingi.Kama kuwapatia makazi, na hata kuuleta muungano kati ya bara na visiwani.
    Katika maisha wahenga wasema ukijua kupata ujue na kukosa. Ila tu maelezo yako ya hapo juu yanaonyesha kuwa kama ulishakataa kushika nafasi hiyo mheshimiwa rais wetu Mwinyi na Mkapa waliyotaka kukupa, Na sasa kwa kukosa nafasi hiyo ya ubalozi unasema uko tayari kuikubali kazi uliyoshaikataa, pamoja na kuwa unasema unaona umeiva sasa! Nafikiri tafsiri yake inaweza kuwa;
    aidha kwa kukosa hiyo uliyokuwa nayo unatapatapa hivyo bora tu chochote kile
    au ni kweli kuwa umeiva na kama hata ungeambiwa uendelee pengine ungekataa na kusema "jamani eh nimefanya hii kazi siku nyingi naomba kulitumikia taifa langu vinginevyo.
    Kwa mawazo yangu mimi ningekushauri kuwa na "subira" hii itakupa heshma na muda wa kuchanganua mambo. nina hakika rais wetu ni mtu makini na bazara lake pia.
    Nina uhakika visiwani hasa pemba wanahitaji mchango mkubwa wa msomi kama wewe ili kusukuma maendeleo yao hasa katika swala la ajira, afya na elimu.
    Kila la Kheri.
     
  • Comment #4 (Posted by KARIM)
    Rating
    Kwa maon iyangu kwanza balozi karume angesafisha jina lake juu ya tuhuma zilizoandikwa na gazeti la Dira kuwa laimuua msichana Zanzibar baada ya kumnajisi na kumtupa jalalani na baadae Mwalimu Nyerere aliokoa Kashfa hii kumhamisha nje na kumpa kazi ya unaibu balozi huko USA.
    Kwa hiyo siasa inataka watu wasafi nafikiri ungesafisha jina lako kwanza.
     
  • Comment #5 (Posted by Hamisi Mapiku)
    Rating
    Mimi nashukuru sana kuona Balozi huyu anamoyo mkubwa sana wa kutaka kuendeleza nchi yake kwani kwa wakati kama huu yeye mwenyewe amekubali na anahaja ya kutaka kugombea cheo chochote cha siasa katika nchi hii kwani waliyo wengi wangetokomea hokohuko wasingekuwa na mpango wowote wa kutaka kuunganika na Watanzania wenzake. Hivyo karibu Tanzania na sisi tupo katika ujenzi wa nchi yetu. watu kama ninyi mko wachache tu. Mengi yasemwayo ni kutaka kuharibu jina lako tu. hilo usijali sana nafasi unayo njoo tuwe pamoja. H Mapiku
     
  • Comment #6 (Posted by hanif)
    Rating
    Mimi personal nafurahi sana kusikia hivyo kwani ni watu au viongozi wachache sana ambao wanamoyo kama huu mimi nampongeza sana asisikilize maneno ya watu kuna watu hawapendi tu kusikia jina la mtu labda likisifiwa kwa mambo mazuri ila hongera sana mzee tunakukaribisha sana znz kwani huu ni muda muafaka wa kuhitaj msaada wako kw wazanzibari. ALL THE BEST
     
  • Comment #7 (Posted by Fuad Mohamed)
    Rating
    Miimi si Mwana siasa, lakini huyu balozi amejieleza vizuru sana na anaonekana wazi anajua kazi yake, kwakweli ni mtu mkweli na wala hana majungu na mtu.kwa upande wangu namuombea kila la kheri kwani sio kua ni balozi tuu huyu Ni mtu aliye soma sana, tena kasoma huko marekani kwenye skuli za kusifika duniani ndiyo alizokwenda yeye na Rais mtaafu bwana Mkapa. Columbia University ambacho ni chuo kinaongoza katika jumuiya ya
    Marekani. kahivyo asiwe na wasiwasi Rais Kikwete ni mtu anaye tambua ni nani ataweza atanisaidia katika kiiongoza Tanzania kwa hakika atampa kazi inayo stahiki kwa mujib
    wa kisomo chake na muda aliotumikia nchi yake. asante sana mungu atakujaalia kila la kheri. Amin.
     
  • Comment #8 (Posted by galloway)
    Rating
    mimi naona hafai kwani ndugu yake ameshaua na yeye ameua sasa unategemea nini bali ataendeleza tu kuua kwani tz sio nchi ya kifalme sasa leo na yeye agembee urais itakuwa vipi kwa maoni yangu naona bora asijiingeze kwenye siasa kwani ndugu yake hakubali domokrasi mbona hajatumia hikma ya kumwambia ndugu yake anavyo fanya wao akina karume wanataka tu kuendeleza udictater tu hana nia nzuri na leo tunaona ndugu yake anavyo fanya
     
  • Comment #9 (Posted by Melkion Komba)
    Rating
    Balozi amejieleza vizuri sana,naona muda wa miaka 14 katika utumishi kwa nyazifa kama hiyo unatosha its infact too much, kunavijana wengi tu hatuna kazi na tunasifa kama zake.apumzike na kwa elimu aliyo nayo nadhani anaweza kurudi zanzibar kuendeleza nchi yake.Kwa maoni yangu hana haja tena yakutaka kuteuliwa kitu kingine afanye shughuli zake binafsi kwa kutumia elimu aliyonayo tuone kama ni mbunifu.Kwamaoni yangu ningependa Rais awaondoe wote waliokaa zaidi ya miaka kumi waje waendeleze nchi yao kwa vitendo na sio maneno tu.Kuwa na uhusianao na nchi tu hakutoshi kusema mtu amefanya kazi nzuri kwa kuwa hatujawahi kuwa na ugomvi na nchi yoyote kama watanzania kwahiyo warudi wote waje waonje uchungu wa kukosekana kwa umeme,maji n.k.wasije wakajisahau huku ughaibuni wakazani ndio Tanzania.
     
  • Comment #10 (Posted by Ally)
    Rating

    Maoni yake ni mazuri, kweli ana degree tatu, kimawazo yangu Ali Karume anasahau hivyo vyeo wanavyopewa siyo kwa kuwa wamesoma bali ni malipo ya CCM. Mimi kwa kifupi simchukulii yeye kama serious politician ambae amekomaa. Pamoja na miaka 14 ya udiplomasia kutoa habari kuwa alishaombwa apewe kazi nyingine inaovyesha dhahiri kuwa hafai kupew kazi ya wadhifa mkubwa. Lakini Umepewa nafasi nyingine baada ya kulalamika.
     
  • Comment #11 (Posted by an unknown user)
    Rating
    asante ccm ipo siku zote. haya sasa hamtaki? ndiyo balozi wenu hivi sasa huko italia!! huyu si mwanasiasa bali ni mtoto wa system na lazima atunzwe.
     
  • Comment #12 (Posted by Hemedi Begge)
    Rating
    Muheshimiwa Balozi Karume kwakuzingatia
    maelezo yako uliyo yatoa katika kipindi
    hiki mim ningeweka wazi kuwa pamoja na Digrii zako 3 ulizonazo kuna kitu kimoja ni muhimu sana kukijuwa.Katika nchi yetu Tanzania nafasi ya juu kabisa
    kiuongozi ni kuwa Rais wa jamuhuri ya
    muungano wa Tanzania.Nafasi hiyo ndiyo
    uliyo ielezea kuwa marais wa awamu mbili zilizopita walikuita ili usimame kugombea kwakiti cha ccm.pamoja na hayo
    nikuwa uliingia katika nafasi ya kugombea na hukupatanafasi kama ulivyo kusudia.Sasa basi kusubiri muhishimiwa Rais wa awamu hii ya nne akupangie kazi ili uiangalie kama hulingani nayo
    kutokana na Digirii zako tatu basi ndiyo ummwambia aa nafsi yangu ya utumishi serekalini imekomea hapa Asante .Mimi naona hii ni sawa na kuwa unamlazimisha Rais akupenfasi ya juu zaidi yaani isiwe kakutoa ubalozi ukawa mkuu wa mkoa yaani hutalitumikia taifa hii ndiyo maana yako.Hii nikusema unataka uwe waziri wa wizara yoyote hapa nchini Tanzania ilimuradi kazi yako isiwe chini yahapo.Kwasisi tusiokuwa na digirii nafikiri utakuwa unatutisha kuwa unajipangia kazi si kuwa upo makini kusubiri kazi utakayo pangiwa.Mtanzania mwenye moyo wa kulitumikia taifa hili la kitanzania haangalii kuwa na elimu kiasi gani ili awekiongozi adha diwani,Mkuu wa mkoa.Mkurugenzi wa wizarafulani .Popote pale utakapo chaguliwa na kiongozi wako wanchi unapaswa upatumikie na kama utakuwa hupawezi basi itaonekanawazi kuwa hupawezi.Sasa kusubiri nafasi ya juu kielimu hii unatuangusha na digirii zako tatu ningeomba uwe na moyo wa kututumikia hata ukiwekwa mkurugenzi wa wilaya kwani pengine ni njia tu unapita kesho Rais atasema njoo hapa utakuwaziri mkuu.Fikiria vema muheshimiwa balozi kaulizako kwani haziowani na imani ya wananchi wa Tanzania pamoja na kututumikia kwa miaka 14 nnje ya nchi kwakuzingatia maelezo yako.Najuwa hukutamka kuwa unataka cheo chajuu lakini maelezo yako yanajiowanisha hivyo muheshimiwa balozi karume.Karibu tuungane nyumbani kulitumikia taifa katika ngazi zote kupanda cheo na kushuku nikitu cha kawaida kabisa wala siyo Siasa.
     
  • Comment #13 (Posted by Mkama Mathias)
    Rating
    Sioni kama ni tatizo, Balozi ametoa yaliyo moyoni na uzoefu wake alionao. Tuna mengi ya kujifunza toka kwake. Binadamu hutofautiana lakini kila mtu anao utashi. Tunapojadili mambo au kuchangia mwenzako anachosema kwanza nasi hatuna budi kupima matendo yetu. Uhuru tulionao usitulemaze. Kwa ujumla Balozi ni mafano wa kuigwa katika kipindi chake licha ya majukumu ya kitaifa ameweza kuitafuta elimu ili imwezeshe kuchanganua mambo.

    Naomba tunapotoa hoja tusimjengee chuki na kiongozi wake wa nchi au kuleta chuki zetu binafsi za majumbani. tuangalie kama anafaa kwa nini asipewe nafasi na bado ni kijana. Tusisahau duniani kote na kwa viongozi wote lazima watateua watu wao kulingana na uwezo wao wa kumudu mambo, kisiasa ili kurahisisha utendaji wao wa kazi na wakati mwingine muda na masharti ya kazi afanyao mtu. Naomba tuwe watafiti kwanza ili tuijenge nchi na siyo kubomoa nchi.
    Haya ni maoni binafsi. Ahsanteni
     
  • Comment #14 (Posted by MPENDA AMANI)
    Rating
    Mimi sioni sababu ya yeye kujisifia kiasi hicho, cha msingi kama yeye kweli anaipenda nchi yake, kama mdau mwingine aliesema ni kurudi nyumbani hata akipewa kazi ya ukuu wa mkoa afanye, lakini inaonekana yeye dhumuni lake ni kutaka kuwa Rais, na ajue kuwa na digrii 3 sio hoja ya kuwa lazima awe raisi, cha kwanza aje akae hapa nchini aone machungu ya wananchi sio kukaa huko ughaibuni na kuanza kudai anataka kugombea nafasi ya urasi wakati hajui hata matatizo ya wananchi yako vipi, adha ya matatizo ya umeme, huduma za afya na mambo mengine. Tunataka viongozi safi wanaojali wananchi na wanaoweza kweli kufuatilia na kujua matatizo
     
  • Comment #15 (Posted by Zacharia Jackson)
    Rating

    Nitaendelea kugombea nafasi za kisiasa- Balozi Karume
    By Habari Tanzania Published 06/30/2006 Habari za Kitaifa Rating:

    Balozi wa Tanzania aliemaliza muda wake nchini Ujerumani Balozi Ali Karume amesema bado hajakata tamaa katika kutafuta nafasi za kisiasa na anakusudia kuomba tena ridhaa ya wanachama wa CCM katika chaguzi zijazo.

    Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake mjini Berlin, Ujerumani Balozi Karume alikiri kuwa aliingia katika kinyanganyiro cha mwaka jana akijua kabisa kuwa nafasi yake ni ngumu sana alihisi ilibidi kuanza pahala.

    Elimu ninayo,nina digrii tatu nimechukua marekani na nashukuru nimeaminiwa na marais wa awamu zote mbili niliofanya nao kazi wamewahi kuniomba kuchukua nafasi kubwa sana katika nchi yetu lakini nilikataa kwa vile nilidhani muda bado, lakini sasa nadhani baada ya kuwa balozi kwa miaka kumi na nne sasa nimewiva na uwezo ninao hivyo sioni kwa nini nisigombee tena

    Alipoulizwa kuhusu mazingira ya uhamisho wake na iwapo kauli ya Ikulu kuwa ´´atapangiwa kazi nyingine´´ pengine ni siasa tu kwa vile kishaondolewa Balozi Karume alisema ameichukulia kauli hiyo vizuri kwa vile anadhani Rais kaamua kutafakari nafasi gani itamfaa zaidi baada ya kuwa nje kwa miaka 14.

    ´´Mimi nimeichukulia positively tu kuwa rais kaamua huyu bwana ngoja kwanza nitafakari wapi aende ana uzoefu mkubwa na pia hakuna haraka kwenye mambo haya´´. Alipobanwa kuwa haoni kuwa kwa kugombea kwake katika uchaguzi wa mwaka jana ndani ya CCM atakuwa amejiwekea mazingira magumu kuweza kufanya kazi ndani ya serikali ya sasa Balozi Karume alikanusha hilo na kusema kuwa kwa sasa ni vyema kusubiri kazi atakayopangiwa iangaliwe kama ataimudu au la ingawa pia aliweka bayana kuwa si kazi zote anazoweza kukubali.

    ´´Mimi ni mwanadamu bwana mwandishi hufika wakati nikaona kabisa hii kazi niliopangiwa kabisa haiendani na kisomo changu na uwezo wangu na rekodi yangu, na ni wazi kuwa nikipewa kazi ambayo nimeiona hivyo nitamwambia mheshimiwa Rais ndugu yangu ahsante sana nadhani utumishi wangu unakoma hapa niendelee na shughuli zangu´´ alisisitiza.

    Aidha akizungumzia nafasi yake kisiasa Tanzania Balozi Karume alisema amewahi kuombwa na marais Mwinyi na Mkapa kutumikia taifa katika nafasi kubwa zaidi ya aliyonayo sasa lakini alikataa kuitikia wito huo kwa vile muda wake ilikuwa bado lakini fursa hiyo ikitokea tena hatosita kuichukua. Hata hivyo alipobanwa kufafanua ni kazi gani hiyo aliyopewa na kuikataa Balozi Karume alikataa kusema na kusema muda ukifika itakuwepo katika kitabu cha kuelezee maisha yake pindi akishastaafu.

    ´´Lakini nikwambie tu kuwa mwaka 1988 pale London unapotoka Rais Mwinyi aliniita kuniomba niifanye kazi hiyo lakini nilikataa kwa nia njema kabisa na hata Rais Mkapa katika kipindi cha pili cha uongozi wake aliniambia niifikirie kazi hiyo lakini niliona muda wake bado, lakini bwana mwandishi nakuthibitishia lau fursa hii ikitokea tena nadhani nimewiva na muda tayari nitafanya, nashindwa siwezi kuweka bayana kwa sasa kwa vile nadhani inabidi nihifadhi haya kwa ajili ya biography yangu ili na wenzangu wajue niliwahi kuombwa kazi kubwa´´ alisisitiza Balozi Karume.

    Akizungumzia juu ya mafanikio ya ubalozi wake nchini Ujerumani alisema anadhani ameongoza vizuri ubalozi hususan katika kipindi cha mpito kuelekea kuhamisha ubalozi kutoka Bonn kuhamia Berlin na pia kuweka mahusiano mazuri na serikali ya shirikisho ya ujerumani na serikali ndogondogo saba kati ya kumi na sita.

    ´´Hakika nadhani katika vitu nitakavyosema naviwacha kama ni changamoto kwa mwenzangu atakaekuja ni kuwa hana budi kuendeleza haya mahusiano manake yamesaidia misaada mingi kupatikana na sina budi kusema sikuweza kuweka mahusiano na serikali ndogo ndogo za majimbo tisa hivyo kama ni kufeli basi labda hii ndio failure yangu´´

    Hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete aliteua mabalozi kadhaa ambapo Balozi Ngemera aliekuwa katika jumuiya ya Afrika Mashariki kama naibu katibu mkuu anaeshughulikia utawala na fedha aliteuliwa kuchukua nafasi ya balozi Ali Karume ambae taarifa ya Ikulu ilisema atapangiwa kazi nyingine.

    Haya ni mahojiano ya kwanza ambayo Balozi Karume amekubali kufanya tangu taarifa ya kuhamishwa kwake ilipotolewa na Ikulu.

    Digrii tatu sio kigezo cha uongozi atazame hivi sasa katika serikali kuna wasomi walomzidi yeye na wanaotambulika Kimataifa sio walohudhuria shule tu.

    Yeye kama anafikira na kweli ana akili za kuchunguza mambo angerudi akafaya jitihada za kuwaunganisha Wazanzibari kwa kuanza yeye mengewe kuomba msamaha kwa aloyafanya pamoja familia yake. Hatutaki ufalme Tanzania.
     
Submit Comment

Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Salehe Mmoro
  8. Ramadhan Semtawa
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.