Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mwanajeshi akutwa na risasi 1,900
Mwanajeshi akutwa na risasi 1,900
By Habari Tanzania | Published  08/4/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Asha Bani


MWANAJESHI wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Henry Mwisongo (28), mwenye namba MT 80186 PT, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akikabiliwa na tuhuma za kupatikana na silaha mbili na risasi 1,982.

Mwendesha Mashitaka Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Charles Kenyella alidai kuwa mshitakiwa huyo alikamatwa na silaha hizo, SMG na nyingine G3 pamoja na risasi hizo, Julai 22 mwaka huu, saa 2.20 usiku eneo la Mwenge Mlalakuwa, jijini Dar es Salaam.

Mshitakiwa alikana tuhuma hizo mbele ya Hakimu Mkazi, Sudi Dimbo na kuiomba mahakama impe dhamana kwa kuwa ni mara yake ya kwanza kutuhumiwa kwa kosa hilo na kwamba amesingiziwa.

Hata hivyo, Kenyella, aliiomba mahakama isimpe dhamana mshitakiwa huyo na kwamba upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Alieleza mshitakiwa amekamatwa na silaha nyingi, hali inayohatarisha usalama wa maisha ya wananchi.

Kenyella, alieleza kutokana na sheria ya usalama wa raia, pamoja na sheria ya kuhujumu uchumi, mshitakiwa anaweza kushitakiwa katika kosa mojawapo kwa kuwa haikujulikana alikuwa anatumia silaha hizo katika shughuli gani.

“Kwa kuwa haijafahamika mshitakiwa alikuwa anamiliki vitu hivyo kwa ajili ya shughuli gani, hivyo nina wasiwasi na mshitakiwa akafunguliwa mashitaka yanayoambata na kuhujumu uchumi au ya kuhatarisha usalama wa raia,” alidai Kenyella.

Hakimu Sundi alikubaliana na maombi ya upande wa mashitaka, hivyo kuamuru mshitakiwa huyo kupelekwa rumande hadi Agosti 20, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa.

Awali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Alfred Tibaigana, alikaririwa na vyombo vya habari kwamba mshitakiwa alikutwa na silaha mbili na risasi 2,593.

Katika kesi nyingine, Thomas Herman (26) na Marton Francis (25), wamefikishwa mahakamani hapo wakikabiliwa na tuhuma za wizi wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh milioni 95, mali ya mwajiri wao, Pendo Dominick.

Mbele ya Hakimu Fimbo, Mwendesha Mashitaka Inspekta wa Polisi, Boniface Erdwin, alidai Julai 27, mwaka huu, saa 10:30 alfajiri, maeneo ya Msasani, Dar es Salaam, washitakiwa walivunja nyumba ya Pendo na kuiba mikufu mitatu ya dhahabu, mikufu miwili iliyotengenezwa kwa madini ya tanzanite, vyote vikiwa na thamani hiyo.

Washitakiwa walikana tuhuma hizo na kurududishwa rumande hadi Agosti 20, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa. Upelelezi bado haujakamilika.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.