HATIMAYE Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza uteuzi wa wagombea wake waliowania nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia ngazi ya wilaya hadi taifa.
Pia chama hicho kimetangaza kurejewa kwa mchakato mzima wa uchaguzi wa ngazi ya mkoa na wilaya katika mikoa ya Mara, Lindi, Kaskazini Unguja, Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya na Wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro.
Matokeo ya mchujo huo yanaonyesha kuwa mchuano mkali katika kinyang’anyiro hicho utakuwa ni kugombea nafasi 20 za wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kwa upande wa Tanzania Bara ambazo zinagombewa na wana CCM wenye majina makubwa wapatao 60.
Miongoni mwa majina makubwa yaliyomo katika kundi hilo la watu 60 yumo Waziri Mkuu, Edward Lowassa, aliyepata kuwa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Abdulrahman Kinana, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale-Mwiru na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, Wengine katika kundi hilo ni Novatus Makunga, Tarimba Abbas, Shy - Rose Bhanji, Juma Kapuya, Hamida Kilua, Lucas Kisasa, John Komba, Makongoro Mahanga, Mohamed, Yakub Mamoon, Wilson Masilingi, Bernard Membe na William Ngeleja.
Wanasiasa wengine ni Salim Chicago, Siwajibu Peter, William Lukuvi, Jack Mwambi, Job Ndugai na George Simbachawene.
Wengine ni Abdul Sapi, Frank Uhahula, Deodorus Kamala, Alhaj Said Kilahama, Nicholous Zacharia, David Mathayo, Aggrey Mwanri, David Holela, Isidore Shirima, Stephen Wassira, Maurus Mhimbira na Prof. David Mwakyusa.
Wanasiasa wengine wawili, Christoher Gachuma na Enock Chambiri, ambao awali walikuwa wakiwania uenyekiti wa Mkoa wa Mara nao pia wameingizwa katika kundi la kugombea nafasi 20 baada ya upinzani mkali baina yao kusababisha vikao vya CCM viamue kuwatoa katika nafasi walizogombea awali ili kuepuka mmeguko katika chama.
Aidha, wengine katika kundi hilo ni Emmannuel Mwambulukutu, Amos Makala, Banda Salim, Jackson Msome, Albogast Godogodo, James Msekela, Constantine Kanyasu na Amos Siyantemi.
Pia wamo Mohamed Mkumba, Idrisa Mtulia, Samwel Wangwe, Andrew Chenge, Jared Kaduga, John Chiligati, Pascal Mabiti, Said Fundikira, Abeid Mwinyimsa, Charles Kagonji, Dk. Ibrahim Msengi, Hassan Ngwilizi na Hashim Msafiri Twakyondo.
Mbali ya kundi hilo, Mwanri pia alitaja orodha ya wagombea 31 waliogombea kupitia vijana ambao watakuwa wakisaka viti 15 vya ujumbe wa NEC kupitia kundi hilo wakiongozwa na Nape Nnauye ambaye ndiye mwanasiasa pekee anayegombea kupitia kundi hilo kwa kipindi kingine cha pili na mbunge wa Viti Maalum, Lucy Mayenga.
Mbali ya Nape na Mayenga, vijana wengine ni: Lusingu, Abdallah Mayomba, Omar Kirati, Zainabu Kawawa, Sixtus Mapunda, Venassa Mugeta, Jerry Slaa, Ashura Suleiman, Neema Mwakabonga na Deogratias Ndejembi.
Wengine ni Edwin Sanda, Malkiado January, Penias Kaindoa, Rajab Katunda, Beno Malisa, Paul Kigirini, Lutengano George Mwalwiba, Sarah Ally, Adela Ng'atingwa, Rose Juma, Magembe, Boniphase Magembe, Pili Jabiri, Jastina Mboneko, Violet Mzindakaya, Raymond Mwangwala, Francis Mtinga, Suleiman Nchambi, Hussein Bashe na Rojas Shemwelekwa.
Kundi la wazazi linagombea na watu mbalimbali wanaoongozwa na wanasiasa kadhaa ambao katika vipindi tofauti walijiunga na CCM wakitokea vyama vya upinzani.
Wanasiasa hao ambao wanaonekana kukwepa kishindo kigumu cha kundi la kwanza la nafasi 20 ni pamoja na Richard Tambwe Hiza, Thomas Ngawaiya, Danh Makanga na Adam Malima.
Wengine katika kundi hilo la wazazi ni; Moses Kabeja, Enock Kalumuna, Selina Mkonyi, Mohammed Nassoro Nondo,, Salim Tambalizeni, Mustafa Yakubu, Mussa Azzan Zungu, Ruth Msafiri, Hennry Shekufu, Richard Nyaulawa, Innocent Kalogeris, Azizi Jawad Aziz, Dickens Shindika, Zainabu Gama, Adam Malima, Stella Manyanya, Athuman Mfutakamba na Mgosi Bakari.
Kupitia Umoja wa Wanawake wa CCM Bara kuna majina mengi makubwa maarufu ya wanawake katika siasa za Tanzania wakiwamo: Halima Mwamuya, Sifa Swai, Asha Bakara, Khadija Kopa, Jacqueline Liana, Anne Makinda, Jane Mihanji, Fatuma Mkwawa, Ritha Mlaki, Kate Kamba, Chonjo Regina, Margaret Sitta, Shamsa Mwangunga, Pindi Chana, Amina Said, Janeth Kayanda, Sakina Kabeza, Anne Malecela, Salome Mbatia, Zakia Hamdan Meghji, Jacqueline Noni na Anna Magowa.
Wengine ni Rehema Nchimbi, Chiku Gawala, Halima Kihemba, Fatuma Kimario, Elizabeth Mwaifwani, Gulzar Sabir, Margareth Mganga, Lydia Boma, Zuhura Mikidadi, Ellen Bogohe, Esther Nyawazwa, Mwanaid Maliki, Zainab Vullu, Esha Stima, Dina Chilolo, Tatu Ntimizi, Aisha Omar Kigoda, Mwantumu Mahiza na Beatrice Shelukindo.
Mwambi katika taarifa yake alisema jumla ya wanachama waliojitokeza walikuwa 2,269, na nafasi zilizokuwa zinawaniwa ni 334.