Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  CHADEMA yawanoa viongozi wake
CHADEMA yawanoa viongozi wake
By Habari Tanzania | Published  07/31/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Tamali Vullu


WAJUMBE wa Kamati Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wamefanyiwa semina ya siku moja kuhusu mpango wa ‘CHADEMA ni msingi - tumaini jipya la Watanzania’.

Semina hiyo iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Haidery Plaza, Dar es Salaam, itafuatiwa na kikao cha siku mbili cha kamati kuu cha chama hicho, kilichopangwa kuanza leo.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, alisema lengo la semina hiyo ni kuwaelimisha wajumbe hao, ili baadaye waweze kuutekeleza mpango huo kwa vitendo.

Alisema lengo la mpango huo ni kuwa na viongozi kuanzia ngazi ya msingi (balozi wa nyumba kumi kumi), kwa lengo la kuimarisha chama.

“Hatua hii inatokana na mabadiliko ya katiba ya chama yaliyofanyika mwaka jana, lengo ni kuwa na viongozi kuanzia ngazi ya msingi,” alisema Dk. Slaa.

Dk. Slaa alisema baada ya semina hiyo, itafuatiwa na kikao cha siku mbili cha kamati kuu ambacho kitapokea taarifa mbalimbali za sekretarieti, kutathmini hali ya siasa nchini na kuweka mikakati mbalimbali ya kuimarisha chama.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.