Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  JK ateua Katibu Mkuu mpya
JK ateua Katibu Mkuu mpya
By Habari Tanzania | Published  07/31/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Mwandishi Wetu


RAIS Jakaya Kikwete, amemteua Mohamed Muya, kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo, ilisema kuwa kabla ya uteuzi huo, Muya alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

Muya anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Solomon Odunga, ambaye amestaafu kazi hivi karibuni baada ya kufikisha umri wa kustaafu.

Wakati huo huo, Rais Kikwete anatarajiwa kulihutubia taifa kesho Agosti mosi, badala ya leo kama ilivyo kawaida yake.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu jana ilisema kuwa hotuba ya rais kwa taifa imeahirishwa kwa siku moja kutokana na vikao vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) vinavyoendelea mjini Dodoma.

Imeelezwa kuwa katika hotuba hiyo atakayoitoa katika Ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma, Rais Kikwete anatarajiwa kueleza na kutoa ufafanuzi kuhusu masuala muhimu ambayo yanawagusa wananchi hivi sasa


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.