Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mbunge astaajabisha
Mbunge astaajabisha
By Habari Tanzania | Published  07/31/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Mwandishi Wetu, Dodoma


MBUNGE wa Biharamulo Magharibi, Phares Kabuye (TLP), jana aliwashtua wabunge na kuamsha hisia zao pale alipoinuka na kudai kuwa wabunge wote walipata ushindi baada ya kutumia rushwa.

Akichangia katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria, Kabuye alisema kuwa hakuna mbunge safi ndani ya Bunge hilo isipokuwa yeye na Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

Aliongeza orodha yake ya watu safi ambao walishinda uchaguzi mkuu uliopita kwa njia safi kwa kumtaja Rais Jakaya Kikwete.

Hata hivyo, Kabuye, ambaye mara nyingi michango yake bungeni husisimua, alijikuta katika wakati mgumu baada ya kauli hiyo.

Kabla ya kurusha bomu hilo, Kabuye alianza kuchangia kuhusu kutokuwapo kwa jengo la Mahakama ya Wilaya ya Biharamulo, ambako hakimu hulazimika kuendesha kesi katika wodi ya wazazi, katika jengo la hospitali iliyoachwa na wakoloni.

Lakini baada ya kauli hiyo, Kabuye alianza kuzungumzia rushwa na kusema: “Rushwa katika siasa. Zamani kuku walikuwa hawajisaidii sehemu wanayolala, lakini akatokea jogoo akajisaidia mahali wanapolala, na kuku wengine wakiwamo vifaranga wakaona kumbe tulikuwa tunahangaika… tunaweza kujisaidia hapa hapa. Wakaanza kujisaidia.”

“Sasa wewe jogoo mwanasiasa unapotoa rushwa unakuwa umejisaidia sehemu tunayolala… humu ndani kama tunachunguza na kuwaondoa wabunge… sidhani kama angebaki mbunge… wabunge walioingia humu wameingia kwa rushwa… hatabaki mtu kasoro mimi… pengine na waziri mkuu na rais,” alisema, hali iliyodhihirika kuwaudhi wabunge wenzake.

“Mnasema mnamuenzi (Mwalimu Julius) Nyerere, halafu mnatumia rushwa… nasema akifufuka humu ndani mtamkimbia wote,” alisisitiza.

Mara baada ya kauli hiyo, Mbunge wa Karagwe, Gosbert Blandes (CCM) alisimama na kutaka mwongozo wa Spika, kuhusu alichotamka Kabuye.

Baada ya hapo, Kabuye alisema: “Hilo nililitegemea. Ninao ushahidi wa watu wa Biharamulo, ninaweza kuwaleta wakathibitisha kuwa sijatoa hata pipi.” Hata hivyo, wakati mbunge huyo akizungumza, wabunge wenzake walisikika wakitamka bila kutumia vipaza sauti wakimtaka afute usemi na aombe radhi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Uratibu), Dk. Batilda Burian naye alilazimika kusimama, kumdhibiti mbunge huyo kwa kutumia kanuni.

Dk. Burian alisema alikuwa amemvumilia kwa muda mrefu Kabuye wakati akizungumza kwa sababu amekuwa akitumia lugha ya kuudhi. Baada ya hapo, Kabuye alisimama na kusema: “Kwa kulazimishwa, naomba kufuta usemi.” Hali hiyo haikuishia hapo, Job Ndugai, Mwenyekiti wa kikao cha jana, alisimama na kumtaka mbunge huyo kuzungumza lugha inayowiana na mazingira ya Bunge, akisisitiza kwa kusema huenda Kabuye aliamka vibaya.

“Mheshimiwa mwenyekiti, si kwamba leo nimeamka vibaya, bali nina uchungu… hata mtu anapofiwa hajui machozi yanatoka wapi… kuna wakati tutafukuzana humu bungeni kwa kusema kwa uchungu,” alisema.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.