Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Serikali yakataa mabadiliko ya katiba
Serikali yakataa mabadiliko ya katiba
By Marshy Abdu | Published  07/28/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
Serikali yakataa mabadiliko ya katiba
na Mwandishi Wetu


LICHA ya madai kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa wa kambi ya upinzani na wanaharakati, serikali imesema haina mpango wa kuanzisha mjadala wa mabadiliko ya katiba ya nchi kwa sasa, imefahamika.

Hayo yalibainishwa jana mjini hapa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, wakati alipokuwa akijibu swali bungeni.

Katika majibu yake, Naibu Waziri Chikawe alisema kuwa mabadiliko yaliyopendekezwa kuhusu katiba, yamekuwa yakitekelezwa taratibu.

Akijibu swali lililoulizwa na Mbunge Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini-CHADEMA) bungeni jana, Chikawe alisema kuwa mapendekezo mengi kuhusu mabadiliko ya katiba yalipendekezwa kupitia waraka wa serikali namba moja wa mwaka 1998 ambao serikali iliutumia kukusanya maoni ya wananchi kuhusu mabadiliko ya sheria.

Chikawe alisema kuwa, serikali inayafanyia kazi mapendekezo hayo na kwamba imekuwa ikirekebisha katiba kwa awamu kuzingatia mapendekezo hayo.

Katika swali lake, Kabwe alitaka kufahamu iwapo serikali haioni sasa ni wakati muafaka wa kuanzisha mjadala wa mabadiliko ya katiba ya nchi, ili pamoja na mambo mengine, kuboresha mfumo wa uchaguzi na hatimaye kuwa na mfumo mchanganyiko wa sasa ‘wape wengi’ na ule unaopendekezwa wa ‘uwakilishi wa uwiano.’
Akiendelea kujibu swali hilo, Naibu Waziri alisema kuboresha mfumo wa uchaguzi ni miongoni mwa masuala ambayo serikali iliyakubali na itaendelea kuboresha sheria kwa kadri hali itakavyoruhusu.

Alibainisha mfumo wa uwakilishi wa uwiano ambao mbunge alikuwa anaupendekeza, umeshaanza kutumika nchini na kusema kuwa hivi sasa wabunge wa viti maalumu wanaingia bungeni kupitia mfumo huo wa uwakilishi wa uwiano.

Hata hivyo, alishauri mbunge huyo kuwa kama raia wa Tanzania, anayo haki ya kufikisha maoni yake au mapendekezo yake kwenye vyombo vinavyohusika, ikiwemo Wizara ya Katiba na Sheria, ili yaweze kufanyiwa kazi wakati muafaka utakapowadia.

Akijibu swali kuhusu serikali inasema nini juu ya hukumu ambayo inaitaka serikali kuleta muswada wa sheria ya kufanya mabadiliko katika katiba na inadhani kutakuwa na madhara gani katika ujenzi wa demokrasia, Naibu Waziri Chikawe alisema serikali haikuridhika na uamuzi huo, hivyo imekata rufaa katika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania.

Alisema kwa sasa haiwezi kujadili suala hilo kwa kuwa bado lipo mahakamani Mabadiliko ya katiba ni moja ya hoja ambazo zinapigiwa upatu na vyama vya upinzani na wanaharakati kwa maelezo ya kuwa katiba iliyopo haiendani na mfumo wa siasa na uchumi ambao Tanzania inaufuata kwa sasa.

Kutokana na serikali kukataa kuandikwa kwa katiba mpya, mapema mwaka huu, wapinzani walichukua hatua ya kuanzisha harakati za kutafuta maoni ya wananchi kuhusu muundo wa katiba ambayo wanadhani inafaa kwa mazingira ya sasa nchini.

Chini ya mkakati huo, vyama hivyo vinadhamiria kuandaa rasimu ya katiba na kuifikisha serikalini, ili ijadiliwe kama mbadala wa katiba inayotumika hivi sasa, ambayo imekuwa ikibadilishwa mara kwa mara.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.