Kijana mmoja Mtondo Gabriel mkazi wa kijiji cha Rusohoko wilayani Kibondo anasakwa na shirika la REDESO kitendo cha utetezi na uzuiaji wa unyanyasaji wa kijinsia kwa kosa la kuwatelekeza baba yake na mkewe mwenye watoto wane.
Mwanasheria wa shirika la REDESO Bi. Edna Kamareki ameeleza kuwa wakati zoezi la utoaji wa elimu kwa umma juu ya vitendo vya unyanyasajio wa kijinsia shirika lake lilibaini kuwepo kwa mama aliyetelekezwa na mmewe huku akiishi na baba mkwe wake.
Bi. Kamareki amefafanua kuwa wakati wakijaribu kumtafuta mume wa mama huyo anayefahamika kwa jina la Advela Benedictor walibaini kuwa alikimbilia katika kambi ya Nduta ambako aliishi na mwanamke mwingine.
Juhudu za kumrudisha yumbani ili aisaidie familia yake zilifanikiwa lakini alipotakiwa kujenga nyumba kwa ajili ya mzazi wake wa kiume ambaye hana mke pamoja na watoto wake wane alikimbia tena bila kufanya hivyo.
Shirika la Redeso baada ya uchunguli limebaini kuwa Bw. Kitondo amekimbilia katika kijiji cha busunzu na limeamua kitumia serikali ya kijiji cha Rusohoko na uongozi wa kata ya Kutahana kuhakikisha kijana huyo anasakwa na kurejeshwa ili aishaidie familia yake.
Shirika la redeso linaendesha mradi wa kushawishi na kutetea wanawake na wananume dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia katika kata za Kitahana na Kasanda wilayani Kibondo mkoani Kigoma.