Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Umeme wa Mbinga kugharimu dola mil 50
Umeme wa Mbinga kugharimu dola mil 50
By Marshy Abdu | Published  07/21/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
Umeme wa Mbinga kugharimu dola mil 50
na Tamali Vullu na Rahel Chizoza, Dodoma


UPANUZI wa umeme wa gridi ya taifa kutoka kituo cha Makambako hadi Songea na kisha kupeleka umeme huo Wilaya ya Mbinga, Namtumbo na Ludewa utagharimu dola milioni 50.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, aliliambia Bunge jana kuwa, upembuzi yakinifu kwa ajili ya mradi huo wa umeme ulikamalika mwanzoni mwa mwaka huu.

Alisema serikali inakamilisha majadiliano na serikali ya Sweden ya kupata fedha za ujenzi wa mradi huo.

Ngeleja alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Pindi Chana (CCM), aliyetaka kujua mradi huo wa umeme utagharimu kiasi gani.

Katika swali lake la msingi, mbunge huyo alitaka kufahamu serikali ina mpango gani wa kupeleka umeme wilayani Ludewa, ili kuwawezesha wawekezaji waone madini ya chuma cha Liganga, dhahabu na makaa ya mawe ya Mchuchuma.

Akijibu swali hilo, Ngeleja alisema serikali kupitia Tanesco inatekeleza mradi wa kuyapatia umeme Makao Makuu ya Wilaya ya Ludewa.

Alisema kazi ya ujenzi wa miundombinu ya umeme ilianza Februari 2006 na ilipangwa kutekelezwa katika awamu mbili. Awamu ya kwanza ilihusisha upimaji wa njia ya kupitisha miundombinu, ujenzi wa sehemu ya miundombinu ya umeme na ukarabati wa jenereta ya halmashauri ya wilaya ambayo awali ndiyo ilikuwa itakayotumika kuzalishia umeme.

Alisema awamu ya pili itahusisha ununuzi na ufungaji wa jenereta mbili zenye uwezo wa KvA 1,250 kila moja ambazo zitawasili katika kipindi cha wiki 55 kuanzia Agosti mwaka huu.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.