Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wakora wavamia watalii, wawapora
Wakora wavamia watalii, wawapora
By Habari Tanzania | Published  07/19/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na David Frank na Ramadhani Swayombe, Arusha


KUNDI la watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamewavamia watalii sita na kuwapora vitu mbalimbali ikiwemo fedha taslimu katika eneo la Mto wa Mbu wilayani Monduli usiku wa kuamkia jana.

Habari zilizopatikana kutoka Mto wa Mbu na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Basilio Matei, zilisema kuwa majambazi hao walivamia loji ya Enoto, ambayo hutumika kama kambi na kumjeruhi mlinzi kwa nondo kichwani kisha kuingia ndani na kuanza kufanya uporaji.

Habari zaidi zinasema watu hao waliokuwa wanane, walifika hapo wakiwa wameficha sura zao kwa kofia maalumu na kumjeruhi mlinzi aliyefahamika kwa jina la Komite Andoro (26).

Mlinzi huyo amelazwa katika Hospitali ya Mto wa Mbu akiuguza majeraha aliyoyapata katika kashikashi hiyo na hali yake inaelezwa kuwa si ya kuridhisha.

Baada ya kufanikiwa kuingia ndani, watu hao walianza kudai fedha kutoka kwa wahudumu wa loji hiyo na baadaye kuingia katika vyumba walivyokuwemo watalii hao na kuwapora mali mbalimbali ikiwemo fedha tasilimu.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda Matei alitaja watalii walioporwa kuwa ni Philipe Trin (47) na Helen Trin (46), ambao ni mtu na mkewe raia wa Ufaransa waliokuwa katika chumba namba B.

Alisema watu hao waliporwa fedha taslimu dola 400 za Marekani, euro 250, cheki za kusafiria, Pasi za kusafiria pamoja na fedha za Tanzania sh 120,000.

Aidha, Kamanda Matei alisema raia hao wa Ufaransa walikuwa na watoto wao katika hoteli hiyo ambao nao paspoti zao zimechukuliwa na majambazi hao lakini hawakudhuriwa mahali popote.

Watali wengine walioporwa walitajwa kuwa ni Kristro Simons (30) na mkewe Katte Simons (30) ambao ni raia wa Australia, ambao nao wameporwa pasi zao za kusafiria, dola za Marekani 1000, fedha za Kiarabu 150 na sh 200,000.

Kamanda huyo alisema mara baada ya kufanya uhalifu huo, majambazi hao walitokomea kusikojulikana na baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa za kutokea kwa tukio hilo, limetuma askari wake wa upelelezi kwenda kufuatilia.

Alisema kikosi hicho cha askari wa upelelezi kinaongozwa na Mkuu wa Kikosi cha Upelelezi Mkoa (RCO), Shilogile na amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa askari hao ili kufanikisha kukamatwa kwa waliohusika katika tukio hilo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.