Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  White Sands Hotel yaiibia DAWASCO
White Sands Hotel yaiibia DAWASCO
By Habari Tanzania | Published  07/14/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Schola Athanas


UONGOZI wa Hoteli ya White Sands Resort umetiwa mbaroni kwa tuhuma za kujipatia huduma ya maji kinyume cha taratibu na kuisababishia hasara Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASCO).

Hali hiyo ilitokea jana wakati polisi walipomchukua mhandisi wa hoteli hiyo, Raamy Shandra na kumpeleka katika kituo kidogo cha Polisi Kawe, baada ya kukiri kujiunganishia maji isivyo halali.

Shandra, alikiri kosa na kueleza sababu za kufanya hivyo kuwa ni nguvu ndogo ya maji katika eneo lao.

Aidha, Meneja wa DAWASCO kituo cha Kawe, Eneliko Mulokozi, aliithibitishia Tanzania Daima kuwa hoteli hiyo ni miongoni mwa wahujumu wa maji kwa muda mrefu kiasi cha kujifungia mota ili kuvutia maji mengi.

“Wametumia njia ya maji tuliyounganisha kwa kukata bomba na kuweka ya mota ya umeme yenye nguvu ya hp2 inayosambaza maji eneo la hoteli na eneo la jirani la Water n’ Wild,” alisema Mulokozi.

Ofisa Uhusiano wa DAWASCO, Badra Masoud, alisema ni lazima waifikishe hoteli hiyo kwenye vyombo vya sheria kwa kuwa wizi wa maji ni tatizo sugu katika Jiji la Dar es Salaam na maeneo jirani.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.