Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Balali: Nimezushiwa
Balali: Nimezushiwa
By Marshy Abdu | Published  07/13/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
Balali: Nimezushiwa
na Martin Malera


GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daudi Balali, amesema hatajiuzulu wadhifa wake kwani madai ya ubadhirifu yanayotolewa dhidi yake ni uzushi na uongo mtupu..

Huku akionekana kujiamini zaidi, Balali alisema: “Niko Comfortable, moyo wangu mweupe, ari yangu ya kazi iko juu kwani tuhuma hizo ni uongo na uzushi mtupu na siwezi kujiuzulu kwa tuhuma zisizo na ushahidi.”.

Balali alitangaza msimamo huo jana katika mkutano maalum na waandishi wa habari, uliofanyika kwenye ofisi za Makao Makuu ya BoT, Dar es Salaam..

Ingawa hakutaja majina ya anaowatuhumu, Balali alisema tuhuma hizo zilizosambazwa kwenye mtandao wa intaneti, zimetokana na watu wenye ugomvi wa kibiashara na kusisitiza kuwa ni uzushi usio na chembe ya ushahidi..

“Tuhuma zote dhidi yangu ni za uongo mtupu. Kwanza sijui zimetoka wapi, nani mtunzi na kwanini amefanya hivyo, hilo tunawaachia wanaofanya uchunguzi na naamini siku moja atajulikana na ukweli utajulikana, lakini mimi siwezi kujiuzulu kwa mambo ya uzushi,” alisisitiza..

Akifafanua kuhusu wafanyabiashara wakubwa, Balali alisema wakati serikali inafanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi, wafanyabiashara nao wamekuwa na mikakati yao ya kibiashara kama walivyozoea zamani. .

Alisema hivi sasa BoT imekuwa makini kuwabana wafanyabiashara wanaokopa kwenye mabenki makubwa ili walipe madeni yao, jambo ambalo zamani halikufanyika kwani walikopa bila kurejesha mikopo, lakini sasa BoT imeamua kuwabana, jambo ambalo limewafanya wajenge chuki kati yao na BoT..

Kuhusu tuhuma za ujenzi wa minara pacha (Twin Tower) iliyojengwa kwa gharama kubwa, alisema BoT bado inaendelea na mchakato wa kubaini gharama halisi ya majengo hayo na kuahidi kulitolea taarifa suala hilo baada ya kazi hiyo kukamilika..

Alisema kashfa ya upanuzi wa majengo ya BoT imekuwa ikiwakumba hata magavana waliopita na hata kashfa ya ujenzi wa majengo hayo chini yake si jambo geni..

Akitolea mfano alisema: “Gavana Charles Nyirabu (marehemu) alikuwa na mpango wa kupanua jengo la BoT, alikumbwa na kashfa kama ya sasa. .

“Alivyokuja Gilman Rutihinda, naye alipanua sehemu ya jengo tunalolitumia sasa, naye aliibuliwa kashfa, akaacha na alipokuja Gavana Idrisa Rashid, akaendeleza ujenzi huo naye alikumbwa na kashfa hiyo hiyo na mimi nilivyoingia mwaka 2000 na baadaye kuanza ujenzi wa ‘Twin Tower’, maneno yameibuka tena,” alisema Balali..

Kuhusu suala la akaunti ya madeni lililoibuliwa bungeni, Balali alisema hana sababu ya kutolea ufafanuzi kwani majibu mazuri yalishatolewa bungeni na Waziri wa Fedha, Zakia Meghji na hata Waziri Mkuu, Edward Lowassa..

Kashfa ya BoT kupitia mtandao wa intaneti, uliibuliwa mara ya kwanza bungeni na Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa (CHADEMA)..

Akichangia maoni ya kambi ya upinzani wakati wa mjadala wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Fedha, Dk. Slaa alisema kambi ya upinzani imefarijika baada ya Waziri wa Fedha kukiri kufahamu taarifa aliyoitoa bungeni kuhusu ubadhirifu mkubwa ndani ya BoT unaomgusa Gavana wa Benki Kuu, pamoja na wafanyabiashara wengine wakubwa akiwemo Mbunge wa Kwela, Dk. Chrisant Mzindakaya (CCM), kupitia kampuni anayoimiliki. .

Dk. Slaa alisema Dk. Mzindakaya alichukua mkopo kwa shughuli za kampuni yake ya SAAFI wa sh bilioni 6.217..

Alisema katika mgawanyo wa mkopo huo, aliomba ‘Overdraft facility ya sh mil. 450 zitakazolipwa kwa miaka 5; mkopo wa sh bilioni 2.8 zitakazolipwa katika miaka mitano; na Dola za Marekani 2.528. Jumla yote ni bilioni 6.217. .

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, fedha zote zilikopwa Benki ya Standard Chartered na Benki Kuu ilitoa (Guarantee) mdhamana wa asilimia 100. Mwaka huu wa 2007, Benki Kuu kutokana na mdhamana huo, tayari imelipa kiasi cha sh bilioni 8.1 kwa niaba ya Mzindakaya na fedha hizo pamoja na riba zinakisiwa kufikia sh bilioni 9.7 hadi sasa (Hati ref. CIBD-14662 ya Mei 24, 2007) na mkopo kutolewa 2005..

BoT ambako Gavana wa Benki ndiye kiongozi mkuu na ndiye mhusika mkuu katika tuhuma zilizotajwa. Hivi sasa deni hilo limehamishiwa TIB ambako Mzindakaya ndiko anakotakiwa kulipia deni la BoT..

Alizidi kupasua kuwa hivi sasa, Mzindakaya ameomba adhaminiwe na BoT mkopo mwingine tena wa sh bilioni 2, mkopo huo uko kwenye hatua ya kujadiliwa na BoT, ama kuidhinishwa ama la..

Kutokana na tuhuma hizo, Waziri Meghji wakati akifanya majumuisho ya hoja yake, alisema serikali imeagiza kuanza kufanyika kwa uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha katika akaunti ya madeni ya biashara ya nje zinazoikabili BoT..

Alikiri serikali kupata taarifa za kuwapo kwa vitendo vya rushwa na nyingine za matumizi mabaya ya fedha katika Benki Kuu. .

Waziri Meghji alisema, tayari alikuwa ameshamwagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali, kuanza uchunguzi kuhusu tuhuma hizo..

Meghji alisema, serikali ilikuwa ikitarajia kukamilisha kazi hiyo na taarifa kamili ya uchunguzi huo kutangazwa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu..

Mbali ya BoT kutuhumiwa kutumia fedha nyingi kuliko inavyostahili katika ujenzi wa majengo yake mapya ya ‘minara miwili pacha’ (Twin Towers), kiasi cha dola za Marekani milioni 30.8 sawa na sh bilioni 40 kinatuhumiwa kufujwa katika akaunti ya madeni ya biashara ya nje..

Taarifa zinaonyesha kuwa, wakopeshaji wa kimataifa kutoka nchi 12 waliingia mkataba wa kusimamia akaunti hiyo na kampuni ya Kitanzania ijulikanayo kwa jina la Kagoda Agriculture Ltd kati ya Septemba na Novemba mwaka jana..

Uchunguzi wa awali wa wakaguzi wa nje wa mahesabu ya akaunti hiyo, unaonyesha kuwapo kwa mazingira yenye utata mkubwa unaozingira makubaliano kati ya wakopeshaji na kampuni hiyo iliyolipwa dola milioni 30.8..

Taarifa za awali za uchunguzi huo zinaonyesha kuwa, BoT ilifikia hatua ya kuipa kampuni hiyo fedha zote hizo ikidai kuingia mkataba na wakopeshaji hao katika mazingira ambayo nyaraka zilizopatikana zinaonyesha kuwa na hitilafu nyingi..

Miongoni mwa hitilafu zilizobainishwa katika uchunguzi wa awali ni, kukosekana kwa karatasi rasmi zenye majina ya kampuni hizo za kimataifa.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.