Na Peter Edson
MHADHIRI Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Haidary Amani, amefikishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kinondoni kujibu shitaka la kutishia kuua.
Akisoma hati ya mashitaka mbele ya hakimu wa mahakama hiyo. Nyigilile Mwaseba, Mwendesha Mashtaka, Inspekta Benedict Nyagabona, alidai mshitakiwa, ambaye ni mkazi wa Kawe, alifanya tukio hilo Juni 30.
Alidai mtuhumiwa alitishia kwa kumpigia simu mlalamikaji Kuluthum Ahmad kuwa atampoteza, akimaanisha kuwa atamuua, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.
Hata hivyo Inspekta Nyagabona alidai kuwa bado haijafahamika chanzo cha ugomvi kati ya mlalamikaji na mtuhumiwa na kwamba upelelezi dhidi ya kesi hiyo unaendelea.
Mtuhumiwa alikana shitaka hilo na kupewa dhamana baada ya kusaini bodi ya Sh300,000 hadi Agosti 30, kesi hiyo itakapotajwa.