Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Makamba aaga Dar
Makamba aaga Dar
By Habari Tanzania | Published  06/29/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yusuf Makamba, amewaaga rasmi wananchi wa Dar es Salaam.

Alisema jana kuwa, wananchi wasiwe na hofu kwani yeye anaondoka katika nafasi hiyo na kwenda kuwaandalia makao kwenye nafasi yake mpya ya ukatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Makamba ambaye aliteuliwa juzi kushika nafasi hiyo, aliaga jana kwenye mkutano wa hadhara alipokuwa akikaribishwa rasmi kwenye Ofisi Ndogo za CCM, Lumumba, Dar es Salaam.

Alisema wananchi wa Dar es Salaam wasiwe na hofu baada ya yeye kuondoka, kwani Rais Jakaya Kikwete atawaletea mtendaji mwingine ndani ya CCM, atakayechapa kazi kwa ufanisi kama alivyofanya yeye.

“Wenye hofu kuwa sitaweza kumudu nafasi hiyo, wasijidanganye kwani kabla ya uteuzi wangu kuwa mkuu wa mkoa, nilitoka ndani ya CCM na sasa nimerudi nyumbani.

“Ndugu zangu nyoka hazeeki, anapofikia umri mkubwa hujivua magamba yake na kurudia ujana… CCM imepata viongozi wapya… kawaida mshale kwake ni porini na mimi ni mshale unaorudi porini ambako nilitoka,” aliongeza Makamba ambaye moja ya sifa zake ni nahau na misemo ya Kiswahili.    

Alitamba kuwa yeye na viongozi wenzake waliochaguliwa ni waadilifu, wenye mapenzi makubwa na chama na wanaojua uchungu wa chama na sio warasimu.

Awali, akizungumza katika hadhira hiyo, Katibu Mwenezi wa CCM, Aggrey Mwanri ambaye pia ni Mbunge wa Siha, aliwatahadhariasha wanachama kwamba wakiona adui anawasifia kwa mazuri waliyotenda, waepukane naye kwani hawatakii mema.

Rais Kikwete kwa upande wake, alisema baada ya kufanikiwa kudhibiti mtandao wa majambazi, kazi hiyo sasa inahamishiwa kwa vibaka na kuahidi kuutokomeza mtandao wa vibaka.

Alisema serikali imefanya jitihada kwa kushirikiana na nchi jirani kudhibiti mtandao wa majambazi, na sasa wanatambua kuwa hawawezi kutamba tena kama awali.

“Sasa nawapa tahadhari wale vibaka wanaofanya wanawake zetu wasipendeze kwa kuvaa vidani vya dhahabu, zamu yao inakuja, ingekuwa vyema kwao wakatafuta shughuli nyingine za kujipatia kipato kwa sababu hatutawavumilia,” alisema Rais Kikwete.

Alisema vijana wanaweza kufanya shughuli nyingine, hasa kipindi hiki ambacho serikali imeamua kwa dhati kuyainua maisha yao, kwa kutoa fedha za mikopo kwa ajili ya kuendeshea shughuli za biashara.

 Rais aliwatoa hofu wananchi kuhusu sh milioni 500 zitakazotolewa na serikali kwa kila mkoa kuwa, pamoja na kuzipitishia kwenye benki, hazitatolewa kwa urasimu.

Alisema fedha hizo zitatolewa na benki kwa utaratibu na masharti ya serikali, na sio masharti na taratibu za kibenki, na lengo ni kuhakikisha kunakuwa na udhibiti wa fedha hizo.

“Tumeamua kuzitoa kwenye mikono ya wanasiasa kwa sababu fedha zilizotolewa mwaka uliopita zilipotea bure na wengine hawakuzirudisha. Nia ya kuzipeleka kwa wataalamu ni kuhakikisha zinadhibitiwa ili wananchi wengi zaidi wanufaike,” alisema


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.