Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Daktari mbaroni akidaiwa kuua
Daktari mbaroni akidaiwa kuua
By Habari Tanzania | Published  07/10/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Mwandishi Wetu


DAKTARI Catherine Mng’ong’o (46) na wenzake watatu jana walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa tuhuma za mauaji ya mfanyabiashara Leonard Chandika.

Pamoja na Dk. Mg’ong’o, watuhumiwa wengine ni mke wa mfanyabiashara huyo, Hilda Kibwana (35), Mtamamchungu Kiemba (44) na Salehe Fundi (55) mhudumu wa Hospitali ya Mwananyamala.

Ilidaiwa mahakamani hapo na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Charles Kenyela, kuwa Juni 24 mwaka huu wakati wa mchana, kwa pamoja na makusudi, katika zahanati ya Caith Med Consultancy ya Tandale Uzuri, watuhumiwa hao walimuua Leonard Chandika.

Baada ya madai ya ACP Kenyela kuhusu watuhumiwa hao mbele ya Hakimu Mkuu Mfawidhi, Sivangilwa Mwangesi, watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo kisheria wa kusikiliza kesi za mauaji.

Katika kesi hiyo namba 16/2007 watuhumiwa hao wanatetewa na Wakili wa Kujitegemea Julius Ndazi. Hata hivyo Hakimu Mwangesi, aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 23 itakapotajwa tena baada ya upande wa mashitaka kudai kuwa, upelelezi wa tuhuma hizo haujakamilika.

Awali, akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jamal Rwambow, alidai kuwa, mfanyabiashara aliyekufa alikuwa na kete 18 tumboni kabla ya kufanyiwa upasuaji na kufariki dunia Juni 24.

Kamanda Rwambow, alisema katika upelelezi huo, polisi imebaini kuwa Juni 18 mwaka huu, marehemu alienda nchini Zimbabwe kupitia Tunduma kwa hati ya kusafiria namba AB. 0331922 iliyotolewa Novemba 25 mwaka jana.

Aidha, katika upelelezi huo, ilibainika kuwa Juni 19 mwaka huu, alilala katika Hoteli ya Blue Water kwa siku moja na Juni 20 na 21 alikuwa nchini Zimbabwe, huko alilala katika Hoteli ya Palm Rock Villa ya mjini Harare.

Kamanda Rwambow, alieleza kuwa Juni 22 marehemu alianza safari kurudi nchini Tanzania kupitia Mbeya kwa basi la Falcon namba T622 AAS na Juni 23 akiwa mjini Mbeya, alibadili usafiri na kupanda basi la Taqbal namba T612 AAN kuja jijini Dar es Salaam.

Akiendelea kutoa taarifa za upelelezi wa kesi hiyo, Kamanda Rwambow alidai kuwa Juni 24 mke wa marehemu alipokea taarifa kuhusu ugonjwa wa mume wake na alipokwenda kumpokea alimfikisha kwenye zahanati binafsi ya Cath Med Consultancy eneo la Tandale Uzuri.

Akiwa kwenye zahanati hiyo alifanyiwa upasuaji na kutolewa pipi 18 za dawa za kulevya zilizokuwa tumboni mwake na kisha kushonwa.

“Jeshi la Polisi linaamini kuwa marehemu alifariki dunia wakati wa upasuaji…kwani baada ya shughuli hiyo, waliuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka katika Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kuuhifadhi.

“Kwa bahati nzuri, tulipata taarifa kutoka kwa wasiri wetu tukafuatilia na tulisitisha shughuli za mazishi muda mfupi kabla ya mwili huo kuzikwa,” alidai Rwambow.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, polisi inaendelea na upelelezi kwa ajili ya kuwakamata watu wengine waliohusika.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.