Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Seleli aapa kuwabana Chenge, Karamagi
Seleli aapa kuwabana Chenge, Karamagi
By Habari Tanzania | Published  07/9/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

*Wabunge wamsubiri Margareth Sitta leo

Na Ramadhan Semtawa, Dodoma

MBUNGE wa Nzega (CCM), Lucas Selelii, amesema bado hajabadili msimamo wake wa kuzibana Wizara za Miundombinu na Nishati na Madini licha ya serikali kutenga fungu kwa ujenzi wa barabara ya kati Dodoma-Singida.

Hatua ya serikali kutenga fungu kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo

imeonekana kuwa ni shinikizo kubwa kutoka kwa wabunge wa kanda ya ziwa ambao wamekuwa na ajenda ya pamoja ya kuibana serikali kutaka barabara hiyo ikamilike na itamke lini itakamilika.

Mawaziri Nazir Karamagi wa Nishati na Madini na Andrew Chenge wa Miundombinu, wanatarajiwa kukabiliana na maswali magumu kutoka kwa wabunge wakati wa kuwasilisha bajeti za wizara zao wiki ijayo, kutokana ahadi nyingi zilizotolewa na serikali kushindwa kutekelezwa.

Akizungumza na gazeti hili juzi, Selelii, alisema katika vitabu vya awali hakukuwa na fungu lolote lililokuwa limetengwa kwa ajili ya uendelezaji wa barabara hiyo ya kati lakini hivi sasa limetengwa.

Hata hivyo, Selelii alipoulizwa kiasi gani cha fedha kimetengwa kwa ajili ya barabara hiyo ambayo yeye amekiona, alijibu, " kuna kitabu kinaonyesha hilo fungu la miradi, ningeweza kukuonyesha, najua kuna matatizo mbele, lakini angalau sasa kuna fungu".

Selelii alipoulizwa tena, msimamo wake wa kutaka kuibana wizara ya Miundombinu ni wa nini wakati tayari ameona fungu limetengwa, alijibu, "sijaona fungu la barabara ya Itigi/Tabora,".

Alisema alipewa ahadi kwamba barabara hiyo ingetengewa fungu lakini hadi sasa haionyeshi kama imetengewa hivyo akaongeza, " Sasa ninataka wanieleze ahadi yao imefikia wapi, patachemka," alisisitiza.

Kuhusu msimamo wake wa kuibana wizara ya nishati na madini, Seleli alisema kwanza ni kuhusu usafirishaji wa mchanga lakini wenye dhahabu ambao umesababisha vijana mbalimbali kukamatwa ikiwemo Nzega.

Alisema taarifa zilizopo zinaeleza kwamba unaosafirishwa ni mchanga lakini imebainika ni dhahabu na tayari kuna baadhi ya watu wamekamatwa kutokana na kosa hilo la kukutwa na dhahabu.

Wiki moja iliyopita Seleli, aliahidi kuzibana baadhi ya wizara, ikiwamo ofisi ya Waziri Mkuu lakini hakuweza kumbana Lowassa katika bajeti yake hadi amemamaliza majumuisho yake.

Naye Ndyesumbilai Florian, anaripoti kuwa wakati bunge likiingia katika wiki ya tano tangu lianze kazi zake mjini Dodoma, leo waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Magreth Sitta atawasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake .

Kivutio kikubwa zaidi pengine katika hotuba ya mwaka huu ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ambayo itawasilishwa Waziri Sitta na hatimaye kujadiliwa kwa siku mbili ni matarajio ya Watanzania kuhusiana na mchango wa sekta hiyo katika maendeleo ya nchi.

Matatizo hayo ya msingi ya walimu ni, mishahara, ajira,malimbikizo ya posho za walimu, azma ya kuwapandisha vyeo walimu wote, hasa wale waliorundikwa katika cheo kimoja kwa muda mrefu.

Pia, kuna tatizo la kufutwa kwa shughuli za michezo katika shule, tangu za msingi, sekondari na vyuo, jambo ambalo lilifanyika wakati wa utawala wa awamu ya tatu, chini ya aliyekuwa Waziri wa Elimu na Utamaduni, Joseph Mungai.

Mungai, ambaye kwa sasa amehamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani, alidai wakati wa kutangaza uamuzi huo wa kufuta michezo, ikiwamo Umisseta, kwamba michezo hiyo ilikuwa ikidumaza utoaji wa taaluma kwa kiasi kikubwa.

Kutokana na hali, macho na masikio ya Watanzania yanawekwa Dodoma ili kuweza kusikia nini kitaweza kuzungumzwa na serikali kwa sasa kuhusu elimu na hata michezo mashuleni, suala la maslahi duni na haki za watumishi, hasa walimu ambao baadhi yao wameamua kukaa kimya, matokeo yake hawatendi kazi kwa moyo kutokana na kukata tamaa.

Sambamba na hilo, suala la ujenzi wa shule za sekondari za kata ambazo zimeenea karibu kila kona ya Tanzania, kiasi cha kuandikisha asilimia 80 ya wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka jana, pia ni suala linalozua mijadala katika jamii.

Kwamba, kwa sasa wapo wanafunzi wengi, ambao katika baadhi ya shule na maeneo kadhaa nchini ambao hawalingani na hali halisi ya walimu.

Pia, suala la msasa ambao umetolewa kwa baadhi ya walimu ama kwa wiki nne au mwaka mmoja badala ya miwili kwa wale wa shule za msingi, nalo linazua hofu.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.