Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kero za kivuko Dar zina mkono wa Mfanyabiashara
Kero za kivuko Dar zina mkono wa Mfanyabiashara
By Habari Tanzania | Published  07/9/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Ramadhan Semtawa

WAKATI usalama wa mali na maisha ya abiria wanaosafiri kati ya Magogoni na Kigamboni jijini Dar es Salaam ukiwa hatarini kutokana na vivuko vya serikali kuwa vibovu, mfanyabiashara maarufu nchini kwa kushirikiana na baadhi ya vigogo wa miundombinu amekwamisha uagizaji wa kivuko cha kukodi cha sh 2 bilioni, akitaka zabuni hiyo apewe yeye.

Kivuko hicho cha kukodi kilipaswa kuingizwa nchini na kuanza kazi Juni 30 mwaka huu, ikiwa ni mbadala wa Mv Kigamboni ambacho kitakwenda kufanyiwa matengezo kwa kipindi cha miaka miwili.

Tayari mchakato wa kupata kampuni hiyo ulikuwa katika hatua za mwisho, lakini mfanyabiashara huyo (jina tunalo) mwenye nguvu na ushawishi mkubwa hadi serikali, ametia mkono na kusababisha Wizara ya Miundombinu kuvuruga mchakato huo.

Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kwamba, hatua ya mfanyabiashara huyo kuitaka zabuni hiyo, imefanya mpango wa serikali kuingiza kivuko Juni 30, kushindikana.

Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, alipoulizwa kuhusu suala hilo mjini Dodoma mapema wiki hii, alisema kuchelewa kuingizwa kivuko hicho kunatokana na kwamba bado kinafanyiwa taratibu za mwisho nje.

Hata hivyo, kauli ya Chenge inapingana na ukweli kwamba taratibu za mwisho za kuingiza kivuko haziwezi kufanyika wakati hata kampuni iliyoshinda zabuni haijajulikana kutokana na kuvurugika kwa mchakato mzima.

Mwananchi imebaini kwamba, makampuni mawili moja ya Uingereza na nyingine ya Uholanzi, ndiyo yaliyokuwa katika hatua za mchuano wa mwisho katika zabuni hiyo.

Kampuni ya Continental ya Uingereza na Seven Sea ya Uhalonzi, ndizo ambazo zimekuwa zikiwania kuingiza kivuko hicho.

Lakini, tangu mfanyabiashara huyo kutaka zabuni hiyo, watendaji ngazi za juu wa wizara wameonekana kugeuka kugawanyika katika makundi, mawili, moja likitaka mchakato uendelee na jingine likitaka uanze upya.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, kundi linalotaka mchakato undelee ni lile la wataalamu kutokana na kuona wananchi wa Kigamboni wako katika hatari kutokana na ubovu wa vivuko vya Mv Alina na Mv Kigamboni.

Kundi ambalo linataka mchakato huo upitiwe upya ni la baadhi ya watendaji wakiwamo kutoka ofisi ya Katibu Mkuu.

Kutokana na hali hiyo, Mwananchi imebaini kwamba, uhakika wa usafiri kwa wananchi wa Kigamboni hadi sasa haujulikani lini utapatiwa ufumbuzi.

Mv Kigambo kwa sasa kipo katika hali mbaya na mara kwa mara kimekuwa kikizimika baharini na kuhatarisha usalama wa mali na raia wanaokitumia.

Waziri Chenge, akizungumzia zaidi hilo, alisema hakuna tatizo la usimamizi wala mvutano ndani ya wizara


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Some people(Leaders) are not concerned with the problem and life of others, what they are suppose to know they are there on behalf of us.
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.