Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Bunda watumia bil. 3.4/- elimu
Bunda watumia bil. 3.4/- elimu
By Marshy Abdu | Published  07/9/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
Bunda watumia bil. 3.4/- elimu
na Mwandishi Wetu


IDARA ya elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, imetumia zaidi ya sh bilioni 3.4 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu na shughuli za maendeleo ya elimu kwa kipindi cha miaka mitano.

Ofisa Elimu wa Wilaya Bunda, Yesse Kanyuma, alisema fedha zilizopokelewa kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu kwa Shule za Msingi (MMEM), kwa kipindi cha kati ya mwaka 2002 hadi Juni 2007.

Kanyuma, alisema katika kipindi hicho, fedha hizo zilijenga nyumba 80 za walimu zilizogharimu sh milioni 456.1; vyumba vya madarasa 426 vyenye thamani ya sh bilioni moja, ujenzi wa vyoo 592 vya wanafunzi kwa gharama ya sh milioni 60 na utengenezaji wa madawati 1,608 kwa sh milioni 100.

Alifafanua kuwa idara ya elimu katika halmashauri hiyo imenunua vitabu vya kiada na ziada vilivyogharimu sh milioni 487.7; ununuzi wa vivunge vya sayansi vyenye thamani ya sh milioni 56.1; tufe na vivunge vya hisabati vilivyogharimu sh milioni 62 huku halmashauri hiyo ikitumia zaidi ya sh bilioni 1.7 kwa ajili ya ruzuku ya uendeshaji wa shule za msingi.

Hata hivyo, amekiri kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na matatizo katika shule za sekondari, hivyo zinahitajika sh bilioni 6 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 673 za walimu kwa shule 24 za wilayani humo huku shule hizo pia zikihitaji jumla ya sh milioni 768 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 192 vya madarasa.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.