Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Serikali Kuu mahakamani
Serikali Kuu mahakamani
By Marshy Abdu | Published  07/6/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
Serikali Kuu mahakamani
Yadaiwa bil. 17/- na mfanyabiashara
na Happiness Katabazi


KAMPUNI ya Khaisa Enterprises Ltd imefungua kesi ya kudai fidia sh bilioni 16.8 dhidi ya serikali kwa madai ya kuvunja mkataba wa kununua helikopta sita za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Kesi hiyo ambayo inaweza kuibua aina nyingine ya kashfa dhidi ya serikali, imefunguliwa jana katika Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.

Wadaiwa katika kesi hiyo namba 74 ya mwaka 2007, ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kwa mujibu wa hati ya madai, fidia hiyo ni sawa na asilimia nane ya kamisheni ya mauzo ya helikopta waliyokubaliana kati ya kampuni ya Khaisa na JWTZ.

Mlalamikaji katika kesi hiyo, anataka alipwe fidia kutokana na kuvunjika kwa makubaliano ya awali ya kutoa huduma ya ushauri wa kitaalamu baina yake na Kampuni ya Eurocopter ya Ufaransa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Pia fidia ya kiasi hicho cha fedha kinatokana na gharama za usafiri alizofanya mlalamikaji nchini Ufaransa, Marekani, Afrika Kusini na Falme za Kiarabu kwa lengo la kuangalia helikopta zilizofaa kununuliwa na serikali kwa ajili ya JWTZ.

Kwa mujibu wa hati hiyo, mwaka 1997, JWTZ ilitangaza kununua helikopta na vifaa vyake toka Paris, Ufaransa katika kiwanda cha Eurocopter ambacho ni kiwanda kikubwa duniani kinachotengeneza ndege za aina ya helikopta.

Barua ya maombi ya kumtaka mlalamikaji atafute helikopta hizo, iliandikwa na Mwanasheria Mkuu Novemba 14 mwaka 1997.

Kutokana na barua hiyo ya maombi, mlalamikaji alienda kuulizia na kuitaka Kampuni ya Eurocopter kuuza helikopta hizo kupitia wakala huyo, kwa ajili ya JWTZ.

“Pande zote mbili katika makubaliano zilikuwa ni wadai kwa nafasi zao, kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Eurocopter. Kwa hiyo katika “Memorandum of Understanding’ (hati ya makubaliano) walikubaliana kimsingi kwamba mlalamikaji ambaye ni kampuni ya Khaisa atapokea kamisheni ya asilimia nane ya jumla ya manunuzi ya bei kama ada ya ushauri katika mwisho wa mkataba wao,” ilieleza hati hiyo.

Kwa mujibu wa hati hiyo, mlalamikaji akiwa katika hatua za mwisho kukamilisha kazi yake, timu ya wataalamu toka ofisi ya Katibu wa Wizara ya Ulinzi, ilikwenda Ufaransa kufanya uchunguzi na kuziona helikopta hizo kabla hazijanunuliwa.

Anadai baada ya uchunguzi kufanywa, wataalamu hao walikubali kuingia mkataba wa manunuzi ya helikopta aina ya COUGAR AS 523 multi-role kwa ajili ya shughuli za kiraia na kijeshi na roketi 1200.

Mlalamikaji ambaye anatetewa na Kampuni ya uwakili ya M&N Law Associate (Advocate), anadai baada ya kuandikwa kwa barua hiyo ya maombi kwa aliyekuwa Mkuu wa JWTZ, Robert Mboma, alisema wanataka Ufaransa itengeneze Cougar AS 532 aina ya helikopta, ambayo itatumika kwa matumizi ya kijeshi na si ya kiraia.

Awali mwaka 1998, JWTZ, iliingia makubaliano na Dar es Salaam-based firm kwa ajili ya kuwapatia helikopta zinazotengenezwa na Kiwanda cha Eurocopter nchini Ufaransa.

Alidai Eurocopter walikuwa wameishaanza kukubali kuuza COUGAR helikopta sita kwa jumla ya sh bilioni 210.

Mlalamikaji anadai kuwa, wakati kazi ya utekelezaji ikianza, alipokea taarifa toka kwa mdaiwa wa kwanza ambaye ni JWTZ, kwamba kampuni nyingine ipo kwenye harakati za kufanya kazi kama yake.

Hata hivyo, alisema barua hiyo haikutaja jina la kampuni hiyo mpya iliyokuwa ikifanya kazi ya kutafuta helikopta.

Hati hiyo ya madai inasema kuwa, kampuni hiyo mpya ilikwenda nje ya nchi na kununua helikopta nne ambazo awali zilikataliwa na wadaiwa kwa madai kwamba hazifai kwa matumzi ya jeshi.

Aidha, anadai kubaini kwamba, helikopta hizo zimenunuliwa kwa gharama kubwa ya dola milioni 9.263 kwa kila moja, tofauti na bei ambayo mlalamikaji alikuwa amekubaliana na JWTZ kwamba kila helikopta ingenunuliwa kwa dola milioni 4.7 na tofauti hiyo ya gharama hiyo ya manunuzi inailetea taifa hasara ya dola za Marekani milioni 4.563.

Hata hivyo, kesi hiyo bado haijapangiwa jaji wala tarehe ya kuanza kusikilizwa.

Taarifa za ununuzi wa helikopta hizo, ziliripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari Mei, mwaka huu ambapo zilidai serikali ilikuwa imeingia mkataba wa ununuzi wa helikopta sita kwa bei kubwa ambazo hazifai kwa matumizi ya jeshi.

Inaelezwa pia kuwa, kampuni iliyoingiza helikopta hizo nchini ni ile iliyonunua ndege mpya ya rais iliyozua mjadala na pia ndiyo iliyoingiza nchini rada ambayo hadi sasa inachunguzwa na Serikali ya Uingereza kwa madai kuwa ilinunuliwa kwa bei kubwa kuliko bei halisi.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.