Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Lowassa; tumejifunza kitu msongamano Dar
Lowassa; tumejifunza kitu msongamano Dar
By Habari Tanzania | Published  07/6/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
TATIZO la msongamano mkubwa wa magari katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na sehemu nyingine nchini limekuwa ni tatizo linaloumiza vichwa vya watumiaji wengi wa barabara akiwamo Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

Kutokana na malalamiko kutoka kwa watu wengi, Machi 9 mwaka huu, Waziri Mkuu aliandikia uongozi wa jiji hilo kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo, na akatumia fursa hiyo kuikumbusha Serikali ya Japan juu ya ahadi yake ya kushiriki katika kutafuta ufumbuzi.

Katika hilo, Lowassa aliiomba Japan ikamilishe utafiti kuhusu upanuzi wa barabara za Jiji la Dar es Salaam na kuharakisha ufadhili wa mradi huo, ili kupunguza msongamano wa magari kama ilivyopata kuahidi siku zilizopita.

Mbali ya hilo, waziri mkuu aliiomba Japan iangalie uwezekano wa kusaidia ujenzi wa barabara za mzunguko jijini Dar es Salaam (The Ring Road Project) na kusisitiza kuwa, endapo suala hilo litapatiwa ufumbuzi, litaokoa muda mwingi wa kazi ambao unapotea barabarani wakati watu wako kwenye foleni ya kwenda ama kurudi kazini.

Kwa maneno yake mwenyewe, waziri mkuu alisema: “Ujenzi wa Ring Road ni muhimu kwetu kwa sababu tunataka kuokoa muda mwingi ambao watu wanaupoteza wanapokuwa kwenye foleni ama wakija kazini ama wakirudi nyumbani.

Pamoja na kupunguza msongamano wa magari barabarani na kuimarisha usafiri wa abiria, Lowassa aliuagiza uongozi wa jiji kusimamia kikamilifu sheria na taratibu za barabarani na kuweka taa sehemu mbalimbali na hasa barabarani.

Tumelazimika kukumbusha mtiririko mzima wa dhamira hii ya Lowassa kwa uongozi wa Jiji la Dar es Salaam ambayo kila mmoja anajua ndiyo iliyozaa utaratibu wa kutumiwa kwa njia tatu kwa magari yanayokuja katikati ya jiji nyakati za asubuhi na yale yanayotoka jioni.

Hata hivyo wakati tukiona manufaa yanayotokana na hatua hizo, hivi sasa Jiji la Dar es Salaam limeshuhudia mabadiliko mengine muhimu ya kupungua kwa misongamano ya magari nyakati za asubuhi na jioni.

Hali hii ya kupungua kwa msongamano kwa watu wanaolifahamu jiji hili, imekuwa ni ya kawaida kabisa miezi hii ya katikati ya mwaka na mwishoni mwa mwaka, wakati wanafunzi wanapokuwa likizo.

Kwa kutambua hilo basi, tunapenda kumuomba waziri mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu, serikali kwa ujumla na uongozi wa Jiji la Dar es Salaam kukitumia kipindi hiki kuanza kufahamu kuwa taasisi za elimu ni moja ya vyanzo vikuu vya misongamano katika Jiji la Dar es Salaam.

Kwa sababu hiyo basi, tunapenda kuviomba vyombo vyetu hivyo vya dola, kuangalia na kutafakari kuhusu umuhimu wa kuendelea kuwa na taasisi nyingi za kielimu kuanzia zile za chini hadi za juu kabisa, katika maeneo ya katikati ya jiji.

Tunasema hivyo tukiamini kwa dhati kabisa kwamba, iwapo serikali itachukua hatua za kuuangalia mwenendo huo na kuutafutia mbadala ama kwa kuendeleza taasisi bora za elimu nje ya jiji au kwa kuhamisha zile zinazowezekana, basi tatizo la misururu mirefu ya magari isiyo ya lazima itapungua sana.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.