SAFARI ya maisha na hatimaye kifo cha Mbunge kijana, Amina Chifupa, kinaelezwa kujumuisha misukosuko, harakati zilizoanza tangu kuzaliwa kwake hadi mauti yalipomfika mwanzoni mwa wiki hii.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwepo maswali kadhaa kwa wananchi wa Tanzania, wanaohitaji kufahamu hasa kiini cha kifo chake huku familia yake ikiwa imeshatoa taarifa kuwa, Amina alifariki kifo cha kawaida kisichohusisha na matukio yoyote yasiyokuwa ya kawaida.
Mmoja wa wanafamilia ya Amina alikaririwa na vyombo vya habari akisema; �mwacheni Amina akapumzike kwa amani. Kifo chake ni kama vifo vya watu wengine, hivyo hakuna haja ya kuzua maswali kuhusu nini kilimsibu kabla ya kufa.�
Maswali yanayotokea katika jamii ni kutokana na tukio la ugonjwa wake kugubikwa na usiri tofauti na yalivyokuwa maisha ya Amina, ambapo jambo dogo alilofanya lilipata nafasi ya kuandikwa ama kwa yeye kulipeleka katika vyombo vya habari au kwa waandishi kulisaka.