Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  ‘Kipanya’ chaua abiria 20 Arusha
‘Kipanya’ chaua abiria 20 Arusha
By Habari Tanzania | Published  06/24/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Ramadhani Siwayombe na David Frank, Arusha


ABIRIA 20 waliokuwa wakisafiri kutoka wilayani Monduli kuelekea mjini Arusha, wamefariki papo hapo baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori.

Ajali hiyo ilitokea jana katika eneo la Meserani Dukabovu, Monduli, majira ya saa nane mchana baada ya gari hilo aina ya Hiace ‘Kipanya’, lenye namba za usajili T 776, ARH kugongana na lori lililokuwa limebeba mchanga.

Taarifa zilizopatikana kutoka kwa watu walioshuhudia tukio hilo na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Matei Basilio, zinasema kuwa, ajali hiyo ilitokea mara baada ya lori la mchanga lililokuwa likielekea Monduli, kutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake na kusababisha ajali hiyo.

Ajali hiyo ilisababisha vifo vya abiria wote 20 waliokuwa kwenye Hiace, akiwemo dereva na kondakta wa gari hilo linalomilikiwa na Muhadi Yusuph, mkazi wa Sakina, Arusha.

Aidha, dereva wa lori lililosababisha ajali, lenye namba za usajili T 377 AGM mali ya Kampuni ya Pilazo Enterprise ya mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro ambaye mpaka sasa jina lake halijafahamika, alikimbia.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani hapa, kazi ya kutambua marehemu waliokuwemo katika Hiace hiyo imekuwa ngumu kutokana na baadhi yao kukatika vibaya sehemu mbalimbali za viungo vya mwili.

Miili ya mabaki na mabaki ya viungo vya marehemu hao hadi jana jioni ilikuwa ikipelekwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kuhifadhiwa na kwa ajili ya utambuzi zaidi kutoka kwa ndugu na jamaa zao.

Kamanda Matei ametoa wito kwa wakazi wote wa mkoani Arusha na maeneo ya jirani, kwenda kutambua miili hiyo na kutaka ushirikiano kuwezesha kumkamata dereva wa lori lililosababisha ajali hiyo.

Wakati tunakwenda mitamboni, baadhi ya waliokufa walikuwa wameshatambuliwa. Hao ni Jimila Juma aliyekuwa dereva na Asifiwe Mohammed, kondakta wa gari hilo.

Abiria waliokufa ni Msee Kimarare, Tumai Deringo, Shazida Juma, Sebastian Sekaja, Stambuli Myovela na Msele Kimario ambao ni askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kutoka Chuo cha Uongozi wa Kijeshi, TMA cha Monduli.

Wengine ni Amina Bitres, Omnyaki Lengoniki, Hamisi Mkumbo na mkewe aliyetajwa kuwa ni Mrs Mkumbo, Nakwetu Mengoriki, George Mashauri na Elibariki Mnzava. Mkumbo alikuwa amechaguliwa kuunda timu ya taifa ya mchezo wa Taekwondo.

Ajali hiyo imetokea ikiwa ni wiki moja na nusu tangu kutokea kwa ajali mbaya mkoani Singida iliyohusisha basi la Mohammed Trans, ambako abiria zaidi ya 25 walifariki katika ajali hiyo, na nyingine iliyotokea hivi karibuni na kuua abiria watatu mkoani Mbeya ikihusisha basi la Kampuni ya SABCO.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.