Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wakimbizi wa Somalia wapewa uraia
Wakimbizi wa Somalia wapewa uraia
By Marshy Abdu | Published  06/21/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
Wakimbizi wa Somalia wapewa uraia
a Mkolo Kimenya

WAKIMBIZI zaidi ya 500 kutoka Somalia wamepewa uraia wa Tanzania baada ya kuishi nchini kwa miaka mingi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Solomon Odunga, alibainisha hayo jana wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wakimbizi Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Odunga alisema wakimbizi hao ambao wanaishi katika Kijiji cha Chogo, mkoani Tanga, walikimbia nchi yao kutokana na vita iliyokuwa ikiendelea na kujikuta wakiishi nchini miaka mingi kinyume cha sheria.

Alisema kutokana na taabu na mateso wanayoyapata wakimbizi kutoka nchi za Afrika ambazo zinaendelea na vita, ni dhahiri kuwa wanapaswa kusaidiwa ili waweze kuendesha maisha yao kama awali na kuwasaidia wengine kurudi makwao.

“Tatizo la wakimbizi si kuwasaidia kwa kuwapa nguo, chakula au kuwahifadhi sehemu, bali ni kuwasaidia ili waweze kurudi katika nchi zao... na ikibidi ni kuwapa uraia wale ambao wanaonekana wana sifa za kupewa,” alisema Odunga.

Alisema ili kulifanikisha jambo hilo, katika nchi nyingine jamii husika inapaswa kulaani vikali vitendo vyovyote vya kulazimisha kwa nguvu wakimbizi kwenda ugenini na badala yake kutoa mwito kukomesha vitendo kama hivyo.

Naye mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mtandao wa Mashirika ya Haki za Binadamu Kusini mwa Afrika, Israel Ilunde, akizungumza katika maadhimisho hayo alisema siku ya wakimbizi ni ishara ya kuheshimu taabu na mateso waliyopata wakimbizi.

Pia alisema siku hiyo inawapa moyo na kuunga mkono maombi na matumaini waliyonayo ya kuweza kurejea nchini kwao siku moja.

Siku ya wakimbizi duniani huadhimishwa kila Juni 20 ya kila mwaka na kaulimbiu ya mwaka huu ilikuwa: ‘Ninatamani kurudi nyumbani siku moja - hivi karibuni.’


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by nyatu)
    Rating
    ni vizuri kiasi,na pia kwa mtazamo wa maoni yangu bado nina mashaka na katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani,kwamba sio raia halisi wa nchini tanzania.
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.