Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Amina Chifupa alazwa
Amina Chifupa alazwa
By Habari Tanzania | Published  06/21/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Mwandishi Wetu


MBUNGE machachari wa Viti Maalumu (CCM), Amina Chifupa, amelazwa katika hospitali moja inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) jijini Dar es Salaam, imefahamika.

Habari za uhakika kutoka ndani ya hospitali hiyo zinasema, Chifupa alipokewa hospitalini hapo juzi usiku kwa ajili ya matibabu ya maradhi yanayomsumbua.

Vyanzo vya habari kutoka hospitalini hapo viliieleza Tanzania Daima jana kwamba Chifupa alikuwa amelazwa katika wodi ya watu maarufu (VIP) alikofanyiwa vipimo kadhaa na muda mfupi baadaye akaanzishiwa matibabu.

Habari zaidi kutoka hospitalini hapo zinaeleza kuwa wodi aliyolazwa mbunge huyo iko katika uangalizi wa karibu, kuliko ilivyo kawaida na watu wasiohusika hawaruhusiwi kufika katika eneo hilo.

Kutokana na hali hiyo, hata baada ya gazeti hili kupata taarifa za ndani kuhusu maradhi yanayomsumbua mwanasiasa huyo, limeamua kutotaja ugonjwa unaomsumbua kwa sasa.

Habari zaidi zinadai kwamba licha ya mbunge huyo kulazwa katika hospitali hiyo, jina lake halijaandikwa kwenye kitabu cha orodha ya wagonjwa na badala yake limeandikwa jina la ofisa mmoja wa jeshi.

“Chifupa kafikishwa hapa jana, na anasumbuliwa na … ila anatibiwa kwa siri kubwa na chini ya uangalizi mkali ambao unazuia hata sisi wafanyakazi wa hapa hospitali kutoikaribia wodi hiyo, labda uwe na shughuli maalumu,” kilisema chanzo chetu.

Hivi karibuni Spika wa Bunge, Samuel Sitta, alilitangazia Bunge kwamba Chifupa ni mgonjwa, ndiyo maana ameshindwa kuhudhuria Kikao cha Bunge la Bajeti kilichoanza mapema wiki iliyopita.

Chifupa, mbunge kijana, amepotea katika macho ya jamii kinyume cha ilivyo hulka yake, tangu habari za kutalikiwa na aliyekuwa mumewe, Mohamed Mpakanjia, Mei mwaka huu ziandikwe katika vyombo vya habari.

Tanzania Daima ndilo lilikuwa gazeti la mwisho kufanya mahojiano na mbunge huyo wakati masuala yake hayo ya ndoa yaliporipotiwa.



How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.