Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mzindakaya asalimisha mabomu, Ngasongwa asongwa bungeni
Mzindakaya asalimisha mabomu, Ngasongwa asongwa bungeni
By Habari Tanzania | Published  06/21/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Kulwa Karedia, Dodoma


KATIKA kile kinachoweza kuelezwa kuwa ni ama kubadilika kwa Mbunge wa Kwela, Dk. Chrisant Mzindakaya (CCM) au kuishiwa mabomu, mwanasiasa huyo jana alitumia muda mwingi bungeni kuitetea serikali dhidi ya tuhuma zilizotolewa na baadhi ya wabunge.

Zama za mbunge huyo maarufu, machachari, mtafiti na mtu aliyewahi kuibua hoja nzito na hatimaye kusababisha mawaziri wajiuzulu, sasa zinaonekana kutokomea.

Akichangia hotuba ya bajeti na ile ya hali ya uchumi bungeni jana, Mzindakaya ambaye hivi karibuni aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo nchini (NDC), alitumia muda mwingi kuipamba serikali.

Katika mchango wake wa jana, Mzindakaya alipinga hoja za wapinzani, na hususan za Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa (Chadema), aliyeelekeza mashambulizi yake dhidi ya Gavana wa Benki Kuu, Daudi Balali, wafanyabiashara na maofisa kadhaa serikalini.

Dk. Slaa wakati akichangia mjadala wa bajeti juzi, alinukuu ujumbe wa barua pepe (e-mail) aliotumiwa ambao ulikuwa ukiwataja viongozi kadhaa serikalini, wafanyabiashara na Gavana wa Benki Kuu (BoT), Daudi Balali kwa kuhusika katika kile kilichoonekana kuwa ni kashfa ya ujenzi wa jengo la minara miwili la BoT.

Katika hoja zake, Mzindakaya alisema madai yaliyomo katika ujumbe huo wa mtandao (Intaneti) unaosema kiasi cha fedha kilichopotea ni dola za Marekani milioni 200 za Marekani, hauna ukweli kwani ukweli ni kwamba, fedha zilizopotea ni Dola za Marekani milioni 131.

Mzindakaya alisema kuna wafanyabishara ambao wamekuwa wakiwatumia wabunge kuwasemea bungeni masuala yao kwa manufaa yao binafsi.

Alisema kwamba anaelewa kuwa suala hilo la BoT linawahusisha Mtanzania na Mzimbabwe na kwamba amefurahishwa na hatua ya serikali ya kufanya uchunguzi wa tatizo hilo.

“Mheshimiwa Naibu Spika, zabuni ya ujenzi wa BoT ilitolewa kwa haki. Kampuni zilizoshiriki kuomba zabuni ni nyingi, lakini walibaki wazabuni sita, Skanska ikashinda kabla ya kujitoa na kumwachia mkandarasi wa sasa na hakuna tatizo kama hilo,” alisema Mzindakaya.

Alisema mwaka 1967, wakati Jengo la Kitega Uchumi la Bima lilipojengwa kwa sh 40,000 kulikuwa na malalamiko mengi ya matumizi mabaya ya fedha, kama inavyotokea sasa kwa BoT.

“Tuliambiwa kuwa tumetumia vibaya fedha za walipa kodi, sasa na suala hili la BoT tunafikiri ni gharama kubwa, lakini Benki Kuu yetu ni safi na ni moja kati ya Benki Kuu 10 bora barani Afrika,” alisema.

Huku akinukuu baadhi ya kumbukumbu alisema; “Mwaka 1995 reserve yetu (akiba yetu ya fedha za kigeni) ilikuwa dola milioni 271, miaka 10 baadaye, reserve yetu ni dola bilioni 2.4. Leo hii ni bilioni 2.2 jamani haya ni maendeleo makubwa kwa nchi,” alisema.

Naye Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki (CCM), amemtuhumu Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, Dk. Juma Ngasongwa, kwa kusema uongo kupitia hotuba yake ya mwelekeo wa hali ya uchumi aliyoitoa bungeni Alhamisi ya wiki iliyopita.

Katika hotuba yake ya taarifa ya hali ya uchumi wa taifa kwa mwaka 2006 na mwelekeo wa muda wa kati (2007/2008-2009/2010), ukurasa wa 48, Dk. Ngasongwa alizungumzia ujenzi wa uzio katika viwanja vya ndege.

Miongoni mwa viwanja vilivyotajwa na waziri huyo kuwa vimejengewa uzio ni Uwanja wa Ndege wa Bukoba, jambo ambalo Balozi Kagasheki alisema halipo.

“Uzio Bukoba hakuna,” alisema balozi huyo wakati akichangia hotuba ya bajeti jana na kuzua minong’ono miongoni mwa wabunge wengi.

Baada ya kumalizika kwa kipindi cha kuchangia hoja asubuhi, baadhi ya wabunge walisema kilichoelezwa na Ngasongwa si cha kweli.

Mmoja wa wabunge kutoka Kanda ya Ziwa, aliiambia Tanzania Daima kuwa, viwanja vya Mwanza na Musoma ambavyo pia vimetajwa na Dk. Ngasongwa kuwa vimepata uzio, navyo havina huduma hiyo.

Katika hotuba yake, Dk. Ngasongwa alisema: “Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2006 baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya mawasiliano ni pamoja na ujenzi wa uzio wa viwanja vya ndege vya Lake Manyara, Musoma, Arusha, Bukoba, Mwanza na Kigoma.

Juzi, hali kama hiyo ilijitokeza tena bungeni baada ya kuzuka malumbano kutokana na hoja ya Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo (CHADEMA), ya kwamba serikali ya awamu ya nne haijajenga hata kilometa moja ya barabara ya lami.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Batilda Burian, alisimama na kutaka Lyimo athibitishe kauli yake, akisema ujenzi wa barabara unaendelea.

Lyimo alisimama na kusema kwenye kitabu cha hali ya uchumi cha Dk. Ngasongwa, kilichoonyeshwa ni ukarabati tu wa barabara, na kwa maana hiyo, serikali ya awamu ya nne haijajenga hata kilometa moja ya lami.

Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, alilazimika kusimama kutoa ufafanuzi, na akasema kumejengwa kilometa 275 za barabara kuu na kilometa 15 za barabara za mikoa. Hata hivyo, ujenzi huo ni wa barabara zilizorithiwa kutoka awamu ya tatu.

Kutokana na hali hiyo, Lyimo alikataa kufuta kauli yake, akisema ukweli ni kwamba hakuna kilometa japo moja iliyojengwa, kwa mujibu wa hotuba ya Dk. Ngasongwa.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by Ohms)
    Rating
    I think Mzindakaya is retarded because the issue is we lost money, and not how much we lost.

    It looks like he wants to look good to the government but based on how stupid his argument is, he is good for nothing.

    How much do you think US 131 M can do for a poor country like Tanzania or any where in the world? He has the gut to call someone who is trying to do his job a liar. Mzindakaya is a hypocrite...he is doing this as a gesture of acknowledgement after given the job of NDC board chairman. He thinks he is helping the government while he is betraying his country, very unpatriotic man and an opportunist. Who is going to pay all this money to the lender? He will be dead when we are struggling to pay back the debt.

    Who sent this kind of fool in the parliament? The pin head is there to kiss ass instead of doing the job people of Kwela wanted him to do. The old fool is the liability to the tax payers, he must go on retirement and he must go now.

     
  • Comment #2 (Posted by lisa david)
    Rating
    hata na mimi sijafurahishwa na kauli tata za mzindakaya, nikiwa ni mmoja wa wanakijiji wa kwela tafadhali lieleze bunge hatuna bababara sumbawanga imekuwa manispaa wakati hakuna kivutio chochote. Please! Mzindakaya angalia tusije kuelewa kuwa unataka uisafishe serikali ili wakupe urais.
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.