WATU 16 waliokufa katika ajali ya basi la Mohamed Trans iliyotokea juzi mkoani hapa, wametambuliwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Luwrance Tarimo aliwataja marehemu hao kuwa ni Mohamed Jafu, Ayubu Kiwanuka, Lucy Maluba, Chris Biseko, Khadala Mayumba, Kimalo Sichumwi, Haruna Siperi na Andrew Mahunde.
Wengine ni Mwanaila Hassan, Martina Mboya, George Winzangi, Monica Mwaputwa, Eaos Bibios, Laitoni Mlokozi, Mutalamila M. na Innocent Beberwa.
Kamanda Tarimo aliwataja baadhi ya majeruhi waliotambuliwa majina yao na ambao wanaendelea na matibabu ni Modi Omari, Gabriel Kaiza Mzirai, Mangera Marwa, Emmanuel Mwiza, Musa Agostino, Laurent Rweyemamu, Bakuna Pagrey, Nickson Ludovick na Paschal Kitengita.
Wengine ni Andrew John, Medrad Eliufoo, George Mabula, Chagu Mapianjo, Musaa Saidi, Paul Joseph, Dk. Adonia Makunja na David Katunga.
Kamanda Tarimo alisema polisi wamegudua kuwa baadhi ya abiria walitumia majina ya watu ambao awali walikata tiketi, lakini baadaye wakaahirisha safari hiyo.