Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wapinzani waiponda bajeti
Wapinzani waiponda bajeti
By Habari Tanzania | Published  06/15/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Mwandishi Wetu


INGAWA wamepewa muda wa siku kadhaa kuisoma na kuitafakari bajeti kabla ya kuanza kuijadili rasmi Jumatatu ijayo, wabunge wameshaanza kuonyesha msimamo wao kuhusu bajeti hiyo.

Kama ilivyotarajiwa, wengi wa wabunge wa upinzani, waliiponda bajeti hiyo, iliyowasilishwa bungeni na Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, jana jioni.

Pamoja na wabunge, bajeti hiyo ilionekana kuzua mjadala mzito pia miongoni mwa wananchi, ambao waliisikia wakati ikiwasilishwa.

Wakizungumza na Tanzania Daima nje ya Ukumbi wa Bunge baada ya kuwasilishwa kwa bajeti hiyo, baadhi ya wabunge walionyesha wasiwasi kuwa huenda ikaongeza gharama na makali ya maisha kwa wananchi, hasa wale wenye kipato cha chini.

Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa (CHADEMA), alisema hajawahi kuona bajeti mbaya kama hiyo, ambayo kwa ujumla wake haionyeshi jinsi ilivyomjali mwananchi wa kawaida.

 “Sijawahi kuona bajeti mbaya na mbovu kama hii, kwa sababu haikuonyesha kuwajali wananchi wenye kipato cha chini, hasa wanaoishi katika maeneo ya vijijini,” alisema Dk. Slaa.

   Alisema bajeti hiyo, inaonyesha kuwa haikuandaliwa kwa ajili ya manufaa ya wananchi, ambao wamekuwa katika lindi kubwa la umasikini na kwamba itakuwa ndoto kufikia kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya kuboresha maisha bora ya kila Mtanzania.

 “Hii ni ndoto ya mchana kwa Mtanzania wa kawaida kufikia  maisha bora kama alivyosema Rais Kikwete wakati akichukua utawala wa nchi hii,” alisema.

Alisema bajeti hiyo imewabana zaidi wananchi ambao watashindwa kununua mafuta hata ya taa kutokana na serikali kupandisha ushuru wake.

 “Watu watashindwa kununua mafuta ya taa, mkaa nao umepanda bei, hali itazidi kuwa ngumu kwa wananchi wa kawaida,” alisisitiza Dk. Slaa ambaye ni naibu kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni.

Hata hivyo, kwa upande wake, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wassira, yeye alisema kuwa bajeti hiyo imeonekana kukidhi mahitaji yote,  kwani imegusa maeneo muhimu.

Mbali na hapo, Wassira alionekana kufurahishwa zaidi na bajeti hiyo kutokana na wizara yake kutengewa kiasi kikubwa cha fedha tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Naye Mbunge wa Musoma Mjini, Vedasto Mathayo (CCM), alisema bajeti hiyo imeonekana kuwakandamiza wananchi kutokana na hatari ya kuwepo kwa kuongezeka kwa bei ya mafuta wakati wowote kuanzia sasa.

 “Bajeti hii imegusa maeneo yote yakiwemo kilimo, madini, elimu na afya, lakini tatizo kubwa lipo kwenye mafuta, ambayo serikali imepandisha ushuru hali ambayo itawabana zaidi wananchi wenye kipato cha chini,” alisema Mathayo.

Naye mbunge wa Jimbo la Mwibara, Charles Kajege (CCM), alisema kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta, wananchi wataendelea kuharibu mazingira kutokana na ukataji wa miti na kuchoma mkaa kwa ajili ya kupata fedha za kujikimu.

Alisema ni wazi kabisa kutokana na hali hiyo, juhudi za kuinua Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupambana na Umasikini (MKUKUTA), hautafanikiwa kwa haraka kutokana na wananchi kubanwa.

Alisema kutokana na hali hiyo, mfumuko wa bei uliopo nchini kwa sasa hauwezi kupungua kutokana na makali ya maisha yanayowakabili wananchi wa vijijini.

Naye Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan (CCM) alisema bajeti iliyowasilishwa ni nzuri kutokana na gesi na umeme jua kupunguziwa kodi.

Alisema hatua hiyo itawawezesha wananchi kununua vifaa hivyo badala ya kusubiri serikali iwapelekee vifaa vya kununua umeme.

Azzan alisema serikali imefanya makusudi kupunguza bei ya vitu hivyo, ili kulinda mazingira kwa sababu wananchi watapunguza matumizi ya mkaa.

Naye Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP), alisema bajeti hiyo ni ngumu sana kwa wananchi wa kawaida, kutokana na kushindwa kutoa mwanga kwao.

Alisema fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa zahanati, shule za sekondari hazitoshi, hali ambayo itafanywa wananchi wakamuliwe kwa kiasi kikubwa cha michango serikalini.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mbunge wa Ismani,  William Lukuvi (CCM), alisema  bajeti hiyo ni ya matumani kutokana na vipaumbele vilivyoainishwa ndani ya bajeti hiyo.

Kuhusu kilimo kupewa kipaumbele, Lukuvi alisema itasaidia nchi kuondokana na tatizo la uhaba wa chakula, na wananchi wataweza kufanya shughuli za maendeleo badala ya kuwa ombaomba kwa upande wa chakuka.

Alisema wafadhili wa nje wakileta fedha kwa wakati, mambo hayo yote yatafanikiwa na mfumuko wa bei kama majanga katika kipindi kilichopita hayatakuwepo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.