Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kondakta afa baada ya kubugia ‘dollas’ na ‘kubel’
Kondakta afa baada ya kubugia ‘dollas’ na ‘kubel’
By Habari Tanzania | Published  05/16/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Esther Katua
 
KONDAKTA amekutwa amekufa ndani ya daladala yake, ikidaiwa kwamba kabla ya kifo alikuwa amekunywa pombe kali aina ya dollas na kubel.
 
Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana alisema jana kuwa juzi saa moja asubuhi dereva wa daladala aina ya Toyota Hiace, lenye namba za usajili T995 ACG, Ali Athuman (30) maarufu kama ‘Kilama’ aligundua kuwa kondakta Stanslaus Vitalis (22) alikuwa amekufa katika gari.
 
Tibaigana alisema Athuman aligundua maiti ya Vitalis ndani ya daladala alipokwenda kulichukua gari hilo mtaa wa Kigoma, wilaya ya Ilala, ili waanze kazi.
 
Alisema kabla kifo chake marehemu alidaiwa kunywa pombe hizo. Maiti ya Vitalis imehifadhiwa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
 
Katika tukio lingine, Tibaigana alisema mtoto Justin Zumbe mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu alitumbukia kisimani jirani na nyumbani kwao, Tabata Kimanga.
 
Kwa mujibu wa baba wa mtoto huyo, Godluck Mbaga (33), wakati mtoto anatumbukia kisimani mama yake, ambaye awali alikuwa naye nje ya nyumba, alikuwa ameingia ndani kwa lengo la kumtayarishia chakula.
 
Tibaigana alisema pia kwamba juzi saa moja na nusu asubuhi kwenye makutano ya Barabara ya Kilwa na Kijichi, daladala Toyota DCM lenye namba za usajili T 862 ABA liliacha njia na kupinduka.
 
Alisema kuwa gari hilo, lililokuwa likiendeshwa na Bashir Said (38), lilisababisha majeruhi 12, ambao walikimbizwa hospitali ya taifa Muhimbili walikotibiwa na kuruhusiwa.
 
Aliwataja majeruhi hao kuwa ni Faida Ahmed (34), Mariam Mzambe (25), Jumanne Abraham (70), Issa Seleman (35), Bakari Kamera (56), Ramadhani Naminga (33), Hamis Lei (44), Harry Ali (23), Aprotus Hyera (39), Riziki Kilimilo (20), Tabu Hamis (28) na Hamis Rashid (34).
 
Katika tukio lingine, moto ulizuka kwenye nyumba ya mtu aliyetambulika kwa jina moja la Shija, Tegeta, mjini Dar es Salaam.
 
Tibaigana alisema kuwa moto huo umeteketeza kila kitu kwenye chumba cha mpangaji, Alex Mwakanyamale (35), vyenye thamani ya shilingi laki 9. Chanzo cha moto huo ni mshumaa uliowaswa na mtoto wa Alex, Jesca (8).
 
Kutoka gazeti la Uhuru

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.