Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Makusanyo sawa, matumizi je?
Makusanyo sawa, matumizi je?
By Marshy Abdu | Published  06/15/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
Makusanyo sawa, matumizi je?
na Mwandishi Wetu


BAADHI ya watu wmeonyesha wasiwasi wao iwapo ahadi zilizotolewa na serikali za kuwapunguzia ukali wa maisha zitatekelezeka ipasavyo, kutokana na ongezeko la kodi mbalimbali kupitia bajeti ya mwaka 2007/08.

Walionyesha wasiwasi huo jana mara baada ya Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, kumaliza kuwasilisha bajeti hiyo bungeni.

Richard Mgaya, aliyejitambulisha kuwa ni mfanyabishara aliyeko Arusha, aliliambia gazeti hili kuwa, bajeti hiyo ina kasoro kubwa ya kushindwa kuelezea matumizi yatakavyokuwa.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu, Mgaya alisema inafurahisha kuona kuwa serikali imeongeza bajeti yake hadi kufikia zaidi ya sh trilioni 6.

Lakini, alisema tatizo si kupata fedha, bali ni udhibiti wa matumizi.

 “Nashangaa sana, katika hotuba yake waziri ameongelea kuhusu mapato tu. Vipi mbona hakugusia matumizi ya fedha tutakazokusanya?” alihoji.

Mgaya alisema kuwa, wasiwasi wake mkubwa ni jinsi fedha zitakazokusanywa kutokana na ongezeko la kodi zitakavypotumika.

 “Tunaweza kujikuta tunakusanya fedha nyingi, lakini tunaweka katika mfuko ambao umetoboka kwa chini, hakitaeleweka kitu,” alisema.

Mfanyabishara mwingine, aliyejitambulisha kama mmiliki wa kituo cha kuuza mafuta, aliliambia gazeti hili kupitia ujumbe mfupi wa simu ya mkononi kuwa, ameshitushwa na ongezeko la ushuru wa mafuta.

Alikuwa akizungumzia ongezeko la ushuru wa mafuta lililotangazwa na Meghji jana la kutoka sh 100 kwa kila lita moja hadi sh 200, ambalo ni ongezeko la asilimia 100.

Katika bajeti hiyo, Meghji aliliambia Bunge kuwa, ili kuongeza uwezo wa Mfuko wa Barabara kumudu ongezeko la gharama za matengenezo ya barabara, serikali inapendekeza kuongeza ushuru wa mafuta ya petroli kutoka sh 100 za sasa kwa lita hadi sh 200 kwa lita.

 “Tangia lini ukasikia kodi ya mafuta ya road toll (ushuru wa barabara) ikapanda kwa asilimia 100?” alihoji mfanyabishara huyo ambaye pia ni msafirishaji.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.